Mchakato wa Yanga uko tofauti kidogo na wa simba, japo lengo la michakato ni kufikia mabadiliko ya kiutendaji.
Mpaka hatua hii ilipofika kwa club ya yanga, bado muwekezaji hajajulikana atakuwa nani.yoyote ananafasi ya kuwekeza kwenye club ya yanga licha ya mchakato kufadhiliwa na GSM.
Mchakato wa simba ulikuwa tofauti kidogo..anaesimamia mchakato wa mabadiliko, tayari amechukua jukumu la kuiendesha club bila mchakato kukamilika. Na ananguvu kiasi cha kuover shadow uwepo wa mwenyekiti wa wanachama wenye asilimia 51. Majority hawamjui hata kwa jina mwenye kiti wa Simba wa sasa.
Kitendo hiki cha MO kuchukua usukani wa club kwa asilimia 100 kabla mchakato haujakamilika ndicho kinacholeta ukakasi kule FCC. Maana anaweza kutumia nafasi yakekutengeneza mazingira yatakayompa favor yeye zaidi wakati xlub inaingia kwenye mabadiliko.
Lakini jambo la pili, ni mchakato wa kumpata mwekezaji. Club ya simba ilitangaza zabuni ya kupata muewekezaji. Masharti ya muewekezaji yalikuwa kwenye tender document, na the highest bidder ndie alitakiwa kupewa timu. MO aliwazidi wenzie kwa kuwekeza bn 20. Ili ushindi wake uwe sahihi, alipaswa kutoa iyo pesa akabidhiwe club. Kitendo cha kusema anapisha ukaguzi wa mali za timu ni kinyume na utaratibu kwa sababu alipaswa kulijua hilo kabla hajasubmit tender document.ili wakati anabid thamani ya uwekezaji wake awe ameshafanya feasibility study ya thaman ya club nakujua bn20 ni sahihi hapa mtu unaweza ukajiuliza alifikiaje bid ya bn 20 wakati hakui thamani ya club, mali na madeni yake.bahati mbaya zaidi mshiriki wa tender anatoa masharti badala ya yeye kuafiki na kutimiza masharti ya tenda.
Kwaiyo, inaonekana alitumia njia yaulaghai kushinda tender na hakuwa tayari kuwekeza. Hii imewanyima fursa wawekezaji wengine, ambao either walibid pesa kidogo, lakini walikuwa tayari kuitoa instantly.
Yanga wanaenda vizuri...so far Mwenyekiti wao bado yuko firm kuongoza club.GSM nao wanabaki kama wafadhili mpaka hatua itakapokamilika.