DOKEZO Waandishi wa Habari Azam wanataabika Mikoani, wanahitaji msaada kulipwa stahiki zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Kuna hii ishu inayowahusu ripota wa Azam TV mikoani, wapo walioanza na kampuni wapo waliojiunga na Azam baadaye. Kwa mujibu wa mikataba yao ambayo ni renewable Kila baada ya Mwaka Mmoja au miaka miwili inatagemeana na maamuzi ya Viongozi, hawa watu ndiyo injini ya habari ya Azam News na baadhi ya vipindi lakini kwa miaka yote hiyo waajiri wamekuwa wakiwafanyia ujanja ujanja kwenye mikataba yao bila kuwapa kile wanachostahili kupata.

Wakati wanaanza kazi Azam Media LTD, taarifa zinadai ya kwamba walikuwa wanalipwa retainer (Mtu anayeajiriwa ili kusaidia au kuhudumia kwa muda mrefu) kiasi cha Tsh. laki tano na elfu hamsini kwa mwezi, na Kila Habari inayoruka kwenye Taarifa za Habari za Azam TV ripota alilipwa kiasi cha Tsh 10 Elfu, na Makala moja ya Dakika 30 Mwandishi Renainer alilipwa kiasi cha Tsh elfu hamsini.

Lakini wakati wa Uongozi wa Tido Muhando akiwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media LTD, walishushiwa viwango vya malipo ambapo Retainer ilishushwa kutoka Malipo ya laki Tano na nusu kwa mwezi Hadi Laki tatu na nusu huku story wakiongeza TSH.elfu 5 na kufikia kiasi cha Tsh elfu 15 na Makala zikishushwa Bei Hadi kufikia kiasi cha Tsh elfu 30 tu.

Lakini Habari zinazoenda kwenye platform nyingine kama Redio ya UFM na Mitandao ya kijamii wakiiipwa kias cha Tsh. elfu tatu tu.

Cha kusikitisha na kuwaumiza zaidi ni kwamba Ili waweze kulipwa stahiki zao kwa mwezi husika kwa maana ya retainer na story zilizoruka, ripota atalazimika kufikisha habari 15 kwa mwezi mmoja huu ni unyonyaji kwa sababu hawa watu hawana likizo, wanafanya Kazi siku zote 365 za mwaka.

Inapotokea ripota akiugua mfano akalala kitandani kwa wiki tatu bila kufanya kazi na kushindwa kufikisha habari 15 hawezi kulipwa stahiki zake, yaani si retainer wala hizo story chache alizozifanyia kazi. Kitu ambacho kwa chombo kikubwa kama Azam ni kuidhalilisha tasnia, na ni Ulukatili na kinyume cha haki za mfanyakazi.

Kama nilivyoeleza hapo awali, baadhi yao wamejiunga na Azam TV kati ya Mwaka 2013 na kuendelea wamekuwa wakipitia manyanyaso makubwa, lakini wale waliopo Ofisini Makao Makuu wanalipwa mishahara minono huku hawa Maripota wakinyonywa mpaka tone la damu licha ya kufanya kazi bila kuchoka kwa muda wote.

Hoja nyingine ni kwamba hao wote kwa miaka yote hiyo inayofikia 10 na zaidi wamefanya bila kuwa na bima za afya wala NSSF ingawa kwa taarifa nilizonazo ni kwamba mwaka jana AZAM Media LTD iliwaunganisha kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii na huduma za bima za afya kwa maana ya NSSF na NHIF ambapo wameanza kuchangia mwezi Julai mwaka huu.

Kampuni inapaswa ione aibu kwa walioanza kuitumikia na kuikuza kwa kuwaingizia michango yao ya NSSF tangu walipoanza kazi. Kuanza kuwalipa ni jambo jema lakini kuanza kuwaingizia NSSF kuanzia mwaka jana baada ya miaka kumi na zaidi ni kutowatendea haki.

Huku ni kuwaonea na kuwapunja haki zao za msingi kwa Maisha yao ya kesho. Fikiria mtu kafanya kazi zaidi ya miaka 10 anaanza kulipwa NSSF mwaka wa 9 yaani miaka yote 9 iliyopita ameambulia patupu hii siyo haki, siyo utu, siyo ubinadamu.

Mzee wetu Said Salim Bakhersa na vijana wake akina Abubakar ni watu wa Imani na wenye hofu ya Mungu tunaamini hawalifahamu hili na hawawezi kukubali kuwapunja vijana waliosaidia kuikuza kampuni yeke kwa kuruhusu mikataba ya kinyonyaji.

Mwisho, hao waandishi hawawezi kusema kwa hofu ya kupoteza vibarua vyao lakini iangalieni upya mikataba ya reporter wenu. Waziri husika wasaidie hawa vijana wapate haki yao, maana kutoingiziwa kitu NSSF kwa miaka zaidi ya 10 ni unyonyaji ambao haujawahi kutokea. Naamini wengi wetu tunaipenda Azam TV kutokana na ubora na umahiri wa waandishi wenu.

Boresheni Maisha yao waendane na hadhi ya Azam TV. Kuna waandishi wenu huku mikoani tunawaona wamechoka mbaya, wengine tunagombaniana nao daladala yaani ni aibu. Unakutana naye kwanza kachoka, nguo mpauko, kavuja jasho wee hadi huruma, kumbe ananyonywa.

Hata akikaa kwenye TV tunaacha kuconcetrate kwenye habari yake anayoichambua tunakumbuka alivyokuwa anagombania chenji na konda ni aibu kwa Kampuni kwakweli.

Vile mnavyopandisha bei za vifurushi wazingatieni na wao kwenye maslahi maana Habari za Azam TV bila wao hakuna kitu. Ikikupendeza Mh. Rais wasemee hawa watu wapate stahiki zao, walipo hawawezi kusema ila wanachopitia wanakijua wenyewe. Mimi nimefanya tu kuleta taarifa.
 
Baada ya vibarua wa viwandani na wa ujenzi, waandishi (reporters) ndio kundi linafuata kwa malipo duni hapa Tz.

Maisha yao ni kuomba tips na kugongea vitu vya bure sababu ya umaarufu.

Matajiri wote wamiliki wa vyombo vya habari hawana utu kabisa. Hao Azam unaowasema, kwa kiasi hicho hicho kidogo ulichotaja wana nafuu kuliko wenzao.

ITV hakuna repota anayefikisha 300,000 kwa malipo yote ya mwezi. Achilia mbali channel 10 na wengine. Mbaya zaidi hakuna chombo binafsi cha habari chenye ofisi mkoani. Reporters wanafanyia kazi nyumbani au kwa malipo hayo hayo kiduchu wanakodi kachumba.
 
Kuna waandishi wenu huku mikoani tunawaona wamechoka mbaya, wengine tunagombaniana nao daladala yaani ni aibu. Unakutana naye kwanza kachoka, nguo mpauko, kavuja jasho wee hadi huruma, kumbe ananyonywa.
Mkuu najua hata wewe utakuwa mmojawapo wa wadau wa media ila unajitoa kuonyesha kama umeipata sehemu hii habari na uhusiki 😂!.

Ila niseme jambo hapa, kwa afrikan private media sijui ni ya nchi gani inalipa vyedi, sijui.

Karibu media zote tabia ipo pale pale, ni vile wengi wanaamua kukomaa tu na eneo walipo ila, hali mbaya sana na ndiyo maana media karibia zote zinaendesha kamari hadi hao Azam.

Shida inaendelea baada ya mwanzo kuonjeshwa asali, media imekaa mahali pake na kuona faida na hasara plus uongozi kuamua kufanya mageuzi kwenye malipo.
 
ili utoke lazime uwe chawa kitu ambacho siwizi

Hii kitu kaitumia Classmate wangu katoboa mapema ingali wengine tunataabika na masomo ya Chuo[emoji23][emoji23]

Anazunguka tu kwenye ziara za Mawaziri, Mjengoni kazoeleka kama kijiwe cha kahawa.

Yote tisa kumi jamaa kaweza kupambana hadi kafikia hatua ya ku Donate mambo ya maendeleo huko kijijini kwao
 
Baada ya vibarua wa viwandani na wa ujenzi, waandishi (reporters) ndio kundi linafuata kwa malipo duni hapa Tz.

Maisha yao ni kuomba tips na kugongea vitu vya bure sababu ya umaarufu.

Matajiri wote wamiliki wa vyombo vya habari hawana utu. Hao Azam unaowasema, kwa kiasi hicho hicho kidogo ulichotaja ndio wanaongoza kwa malipo 'bora' kuliko wenzao. ITV hakuna repota anayefikisha 300,000 kwa malipo yote ya mwezi. Achilia mbali channel 10 na wengine.
Bila Shaka TBC watakuwa wapo vizuri kwenye malipo maana hao ni Gavo
 
Kuna hii ishu inayowahusu ripota wa Azam TV mikoani, wapo walioanza na kampuni wapo waliojiunga na Azam baadaye. Kwa mujibu wa mikataba yao ambayo ni renewable Kila baada ya Mwaka Mmoja au miaka miwili inatagemeana na maamuzi ya Viongozi, hawa watu ndiyo injini ya habari ya Azam News na baadhi ya vipindi lakini kwa miaka yote hiyo waajiri wamekuwa wakiwafanyia ujanja ujanja kwenye mikataba yao bila kuwapa kile wanachostahili kupata.

Wakati wanaanza kazi Azam Media LTD, taarifa zinadai ya kwamba walikuwa wanalipwa retainer (Mtu anayeajiriwa ili kusaidia au kuhudumia kwa muda mrefu) kiasi cha Tsh. laki tano na elfu hamsini kwa mwezi, na Kila Habari inayoruka kwenye Taarifa za Habari za Azam TV ripota alilipwa kiasi cha Tsh 10 Elfu, na Makala moja ya Dakika 30 Mwandishi Renainer alilipwa kiasi cha Tsh elfu hamsini.

Lakini wakati wa Uongozi wa Tido Muhando akiwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media LTD, walishushiwa viwango vya malipo ambapo Retainer ilishushwa kutoka Malipo ya laki Tano na nusu kwa mwezi Hadi Laki tatu na nusu huku story wakiongeza TSH.elfu 5 na kufikia kiasi cha Tsh elfu 15 na Makala zikishushwa Bei Hadi kufikia kiasi cha Tsh elfu 30 tu.

Lakini Habari zinazoenda kwenye platform nyingine kama Redio ya UFM na Mitandao ya kijamii wakiiipwa kias cha Tsh. elfu tatu tu.

Cha kusikitisha na kuwaumiza zaidi ni kwamba Ili waweze kulipwa stahiki zao kwa mwezi husika kwa maana ya retainer na story zilizoruka, ripota atalazimika kufikisha habari 15 kwa mwezi mmoja huu ni unyonyaji kwa sababu hawa watu hawana likizo, wanafanya Kazi siku zote 365 za mwaka.

Inapotokea ripota akiugua mfano akalala kitandani kwa wiki tatu bila kufanya kazi na kushindwa kufikisha habari 15 hawezi kulipwa stahiki zake, yaani si retainer wala hizo story chache alizozifanyia kazi. Kitu ambacho kwa chombo kikubwa kama Azam ni kuidhalilisha tasnia, na ni Ulukatili na kinyume cha haki za mfanyakazi.

Kama nilivyoeleza hapo awali, baadhi yao wamejiunga na Azam TV kati ya Mwaka 2013 na kuendelea wamekuwa wakipitia manyanyaso makubwa, lakini wale waliopo Ofisini Makao Makuu wanalipwa mishahara minono huku hawa Maripota wakinyonywa mpaka tone la damu licha ya kufanya kazi bila kuchoka kwa muda wote.

Hoja nyingine ni kwamba hao wote kwa miaka yote hiyo inayofikia 10 na zaidi wamefanya bila kuwa na bima za afya wala NSSF ingawa kwa taarifa nilizonazo ni kwamba mwaka jana AZAM Media LTD iliwaunganisha kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii na huduma za bima za afya kwa maana ya NSSF na NHIF ambapo wameanza kuchangia mwezi Julai mwaka huu.

Kampuni inapaswa ione aibu kwa walioanza kuitumikia na kuikuza kwa kuwaingizia michango yao ya NSSF tangu walipoanza kazi. Kuanza kuwalipa ni jambo jema lakini kuanza kuwaingizia NSSF kuanzia mwaka jana baada ya miaka kumi na zaidi ni kutowatendea haki.

Huku ni kuwaonea na kuwapunja haki zao za msingi kwa Maisha yao ya kesho. Fikiria mtu kafanya kazi zaidi ya miaka 10 anaanza kulipwa NSSF mwaka wa 9 yaani miaka yote 9 iliyopita ameambulia patupu hii siyo haki, siyo utu, siyo ubinadamu.

Mzee wetu Said Salim Bakhersa na vijana wake akina Abubakar ni watu wa Imani na wenye hofu ya Mungu tunaamini hawalifahamu hili na hawawezi kukubali kuwapunja vijana waliosaidia kuikuza kampuni yeke kwa kuruhusu mikataba ya kinyonyaji.

Mwisho, hao waandishi hawawezi kusema kwa hofu ya kupoteza vibarua vyao lakini iangalieni upya mikataba ya reporter wenu. Waziri husika wasaidie hawa vijana wapate haki yao, maana kutoingiziwa kitu NSSF kwa miaka zaidi ya 10 ni unyonyaji ambao haujawahi kutokea. Naamini wengi wetu tunaipenda Azam TV kutokana na ubora na umahiri wa waandishi wenu.

Boresheni Maisha yao waendane na hadhi ya Azam TV. Kuna waandishi wenu huku mikoani tunawaona wamechoka mbaya, wengine tunagombaniana nao daladala yaani ni aibu. Unakutana naye kwanza kachoka, nguo mpauko, kavuja jasho wee hadi huruma, kumbe ananyonywa.

Hata akikaa kwenye TV tunaacha kuconcetrate kwenye habari yake anayoichambua tunakumbuka alivyokuwa anagombania chenji na konda ni aibu kwa Kampuni kwakweli.

Vile mnavyopandisha bei za vifurushi wazingatieni na wao kwenye maslahi maana Habari za Azam TV bila wao hakuna kitu. Ikikupendeza Mh. Rais wasemee hawa watu wapate stahiki zao, walipo hawawezi kusema ila wanachopitia wanakijua wenyewe. Mimi nimefanya tu kuleta taarifa.
Hao wanajiita sijui Kina Balile akina Kibanda wapo bisy kuisifia serikali na kumkosoa waziri Slaaa ,
Niwape Taarifa Slaa hataki shobo ,wala hatakagi sifa huyo ,anatosha kujisifu mwenywe

teteeni hwa waandishi wa habari wa AZAM kama kweli mnaipenda tasnia na nyinyi sio wabnafsii
 
Back
Top Bottom