Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kamati Kuu ya Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, imewataka wandishi wa habari wote wa Mkoa huo kutoshiriki shughuli yoyote ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mpaka pale Kamati Kuu ya Chama hicho kitakapomaliza tofauti za pande zote mbili.
Taarifa ya leo Machi 15, 2025 iliyotolewa na Kamati Kuu ya Mbeya Press Club (MBPC) imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kufuatiwa madai ya fedha ambayo wandishi wa habari wanakidai Chama hicho tangu Februari 7, 2024 ambapo hati ya madai iliwasilishwa baada ya makubaliano ya pande hizo mbili.
Kamati Kuu ya Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, inawataka wandishi wa habari wote wa Mkoa huo kutoshiriki shughuli yoyote ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mpaka pale tutakapomaliza tofauti za pande zote mbili.
Uamuzi huu umefikiwa kufuatiwa madai ya fedha ambayo wandishi wa habari wanakidai Chama hicho tangu Februari 7, 2024 ambapo hati ya madai iliwasilishwa baada ya makubaliano ya pande hizo mbili.
Madai hayo ni posho za wandishi walioshiriki kwenye Ziara ya siku mbili ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda.
Mwandishi yeyote ambaye atashiriki kwenye shughuli za Chama hicho, atachukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kutoshiriki kwenye tatizo lolote ambalo litamkuta.
Waraka huu ni kwa wandishi wote bila kujali ni wanachama wa MBPC ama sio mwanachama. Asanteni.
Imetolewa na:-
Kamati Kuu ya Mbeya Press Club (MBPC),
Machi 15, 2025.
Mbeya