ze-dudu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 17,640
- 22,748
Hii nchi inachekesha sana ujue[emoji3]Hiyo habari ya kuwa kontena mwenye nazo hajulikani hajitokeze ni uongo.
Kontena kabla ya kusafirishwa melini lilipotoka walitengeneza Bill of Lading (Risiti ya mzigo) ambayo inaonyesha mzigo umetoka wapi,tarehe ya kupakia,mzigo unapoenda, idadi ya mzigo, mmiliki wa mzigo na nani atakayepokea kwa niaba ya mmiliki(notify part ambapo anakuwa ni clearing agent mwenye mzigo na address yake inawekwa).
Hapo mwenye kontena anajulikana direct wamfuate wamwambie afanye taratibu zake.
Nahisi izo kontena ni za bosi mmoja huko serikalini