Waandishi wa habari wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wanawake

Waandishi wa habari wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wanawake

Joined
Oct 26, 2024
Posts
10
Reaction score
0
Zanzibar

1750255579909.png



Na, Zurima Ramadhan

Waandishi wa habari wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wanawake wanaowania nafasi za kisiasa kwa kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili dhidi yao vinatolewa taarifa na kushughulikiwa ipasavyo.

Ameyasema hayo, mkurugenzi wa chama cha wandishi wa habari wanawake tanzania zanzibar (tamwa znz ) dk mzuri issa katika mafunzo ya siku moja, yaliyofanyika katika ofisi ya chama hicho huko tunguu ambayo yamewashirkisha waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari nchini.

Amesema kuelekea kipindi cha uchaguzi wandishi wa habari wana jukumu kubwa la kufanya kazi yao ya ulinzi ili kuwalinda wagombea wanawake watakaogombea nafasi mbali mbali za uongozi dhidi ya vurugu na udhalilishaji unaotokea katika kipindi hicho.

Aidha amewataka wandishi wa habari kuendelea kuandika habari za wanawake waliopata mafanikio katika nafasi za uongozi ili iwe mfano mzuri kwa wanawake wanaotia nia ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Afisa kutoka TAMWA Zanzibar Khairat Haji, amewataka waandishi wa habari kushirikiana na asasi za kiraia kwa kufuatilia, kuripoti na kuelimisha jamii kuhusu ukatili wa kijinsia, hasa unaolenga wanawake katika uongozi.

Nao baada ya waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema wataihamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi na pamoja na kuibua changamoto zinawakabili wanawake katika siasa.
 
Back
Top Bottom