Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Waandishi nguli wa habari za michezo kutoka sehemu mbalimbali duniani wameendelea kuvutiwa na uzuri wa vivutio vya utalii nchini Tanzania baada ya kufanya utalii wa baluni katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kujionea mandhari ya kuvutia wakiwa angani.
Kupitia utalii huo, waandishi hao wamepata fursa ya kushuhudia uzuri wa kipekee wa Serengeti wakiwa juu, wakitazama mandhari ya kuvutia ya hifadhi hiyo maarufu duniani pamoja na utajiri wa rasilimali za wanyamapori zinazopatikana nchini.
Waandishi hao wapo nchini Tanzania kwa ziara maalumu yenye lengo la kujionea utayari wa nchi kuelekea mashindano ya AFCON 2027, sambamba na kutembelea na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania kwa hadhira ya kimataifa.
Ziara hiyo ni fursa muhimu ya kuitangaza Tanzania kimataifa, kuunganisha michezo na utalii, pamoja na kuhamasisha wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kujionea maajabu ya nchi yetu.