Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu habari yenu
Kuna jambo ameongea Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akitahadharisha kuhusu athari ya teknolojia katika tasnia ya habari nchini, akisema inaweza kusababisha kuibuka kwa watu wasio na ujuzi wa kitaaluma "makanjanja" wanaoeneza taarifa za propaganda. Akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) mjini Singida, alisema hali hiyo inahatarisha tasnia ya habari, ambayo ni mhimili muhimu wa taifa.
PIa, Soma: Prof. Adolf Mkenda: Tasnia ya habari iko hatarini kwa makanjanja
Kwa mtazamo wangu, ni wazi kwamba changamoto za maadili katika tasnia ya habari zinatokana na mambo mengi zaidi ya maendeleo ya teknolojia ikiwa ni pamoja na madeni yatokanayo na malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi kwenye hivi vyombo, hali ambayo inadumaza tasnia na kuifanya ioekane ya kawaida licha yakuchukuliwa kama muhimili wa nne wa taifa.
Wamiliki wa vyombo vya habari wana wajibu mkubwa katika kuimarisha maadili ya tasnia hii, lakini wanapoacha kulipa mishahara kwa wakati au kulimbikiza madeni kwa watumishi wao, wanawaweka waandishi/watangazaji katika hali ngumu inayoweza kuathiri weledi na ari yao ya kazi.
Baadhi ya waandishi na watangazaji wamelazimika kukatisha ndoto zao au hata kuacha kazi kabisa kutokana na gumu wa maisha kisa madai ya mishahara yao, pia hata mafao vyombo vingi vya habari havizingatii hilo jambo ambalo linadhoofisha tasnia kwani wengi hujiona kama tasnia ni gunia la misumari.
TCRA ina jukumu muhimu la kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinavyopata leseni vinatimiza dhamira ya kuanzisha na kuendesha chombo cha habari kwa misingi ya taaluma, na si tu kuwa na lengo la kujipatia mapato ya kodi. Ufuatiliaji wa kina unahitajika ili kuhakikisha vyombo hivi vinaendeshwa kwa uwazi, kwa kuzingatia maadili, na kwa kutoa mazingira bora kwa waandishi wao. Hatua hizi zingeweza kusaidia kupunguza tatizo la kuzalisha “machawa” au “makanjanja,” ambao mara nyingi hujiingiza kwenye taaluma bila weledi wa kutosha.