Vyombo vya kimataifa vilivyoalikwa na IEBC kuwa waangalizi wa mchakato mzima wa uchaguzi Kenya 2022, vimetoa pongezi kwa jinsi mchakato mzima kuwa kuelekea uchaguzi na zoezi la upigaji kura, utangazaji matokeo pia vyombo vya ulinzi na usalama kutekeleza wajibu wao bila kuegemea upande.
IGAD, COMESA, EAC, AU, Jumuiya ya Commonwealth n.k wametoa ripoti yao ya awali ya uangalizi kuhusu zoezi zima la uchaguzi wa Kenya 2022 na kuridhishwa namna zoezi zima linavyokwenda.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa niaba ya EAC pia ametoa ripoti kwa niaba ya waangalizi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kiongozi mkuu wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Africa Mashariki Mzee Kikwete amesema uchaguzi umekwenda vizuri matatizo yaliyojitokeza yalitatuliwa mapema na wahusika.
88% ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wakati