Waarabu wawe wanatuwakilisha World Cup, wana uchungu sana kuliko sisi weusi

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Morocco imeingia semi final kwa jasho na damu, wakicheza kwa nidhamu ya hali ya juu, namna wanavyocheza unapata hamasa kuwapigania na kuwaombea kwa mungu wapeperushe bendera ya africa.

Wakat umefika sasa kwa sababu imeonekana akina Senegal, Cameroon na Ghana hawako serious, tuwapeleke sasa akina Egypt, Algeria na waraabu wengine wakatuwakilishe, ingawa Tunisia waliondolewa lkn sio kama Cameroon au Ghana, pumbavu kabisa

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Waarabu hii world cup iko kwao..Wana local fans wanawashangilia na kuwaongeza nguvu ..usitegemee world cup ikifanyika ulaya watacheza "jihad" hivi.....hata Egypt au Algeria wangekuwepo pengine wangeenda mbali zaidi
Tunisia?
 
Tofauti yetu na wao sisi tunaita wachezaji kwa kutoza pesa ila wao wanachagua wachezaji kwa kuangalia uwezo na juhudi, sisi mpaka mchezaji atoe pesa ndiyo aitwe achaguliwe timu ya Taifa, rejea kwa mbape baba yake aliombwa pesa na Chama cha mpira wa miguu cha Cameroon ili mtoto wake achaguliwe timu ya taifa
 
Mfumo uliopo sasa hivi mbona ndio mzuri, hakuna timu kubebwa,
Hao akina Senegal, Cameroon walizitoa timu za kiarabu ndio wakaenda, hawakupewa nafasi, walizitwaa
Halafu hakuna timu ya kiarabu iliyowahi kufika robo fainali kabla ya Morocco
 
Hakuna kitu kama hicho. Tunisia pia amekua good hajafungwa thou ila hajafika huko. Mbona 2010 pale South Africa waafrika walikua tia maji tia maji kama kawaida.

Qatar alikua pale, Saudi Arabia alikua pale, Iran alikua pale ila wako wapi ama walifika wapi
 
Swala sio mashindano kufanyikia kwenye ardhi ya waarabu kwani hao wenyeji sio waarabu na Saudi Arabia sio waarabu.

Morocco wako highly disciplined na pia wachezaji wao wengi ni professionals. Timu zingine za Afrika zilizo tolewa mapema hawakuwa na game discipline kama Morocco.
 
Mfumo uliopo sasa hivi mbona ndio mzuri, hakuna timu kubebwa,
Hao akina Senegal, Cameroon walizitoa timu za kiarabu ndio wakaenda, hawakupewa nafasi, walizitwaa
Halafu hakuna timu ya kiarabu iliyowahi kufika robo fainali kabla ya Morocco
Mimi tokea nimeanza tazama kombe la Dunia waarabu hawajawahi toboa makundi..since 98..huu mwaka Liko nyumbani ndio maana wamekaza..ni kama south Korea 2002...
 
Tofauti yetu na wao sisi tunaita wachezaji kwa kutoza pesa ila wao wanachagua wachezaji kwa kuangalia uwezo na juhudi, sisi mpaka mchezaji atoe pesa ndiyo aitwe achaguliwe timu ya Taifa, rejea kwa mbape baba yake aliombwa pesa na Chama cha mpira wa miguu cha Cameroon ili mtoto wake achaguliwe timu ya taifa
Ni kweli. Koneksheni ndio tatizo. Nilikuwa nashangaa kwa nini kocha wa Ghana anawang'ang'ania Jordan na Andre Ayew waanze kucheza. Kwani hakukuwa vipaji vipya tangu kombe la Dunia lililopita!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Morocco imeingia semi final kwa jasho na damu, wakicheza kwa nidhamu ya hali ya juu, namna wanavyocheza unapata hamasa kuwapigania na kuwaombea kwa mungu wapeperushe bendera ya africa.

Wakat umefika sasa kwa sababu imeonekana akina Senegal, Cameroon na Ghana hawako serious, tuwapeleke sasa akina Egypt, Algeria na waraabu wengine wakatuwakilishe, ingawa Tunisia waliondolewa lkn sio kama Cameroon au Ghana, pumbavu kabisa

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
Ndiyo kanuni za kufuzu zinataka hivi, au umeamua kuja tu na mawazo yako?
 
Back
Top Bottom