Waasisi wa CCM

Waasisi wa CCM

Watu watano muhimu sana katika historia ya uasisi wa CCM ni hawa:
1: Mwalimu Julius K. Nyerere
2: Sheikh Aboud Jumbe
3: Sheikh Rashid M. Kawawa
4: Sheikh Thabit Kombo
5: Mhe. Pius Msekwa

Inabidi CCM iwe na utaratibu wa kuwaenzi watu hawa kama waasisi wa taasisis yao.
Hayati Karume walikuwa wameshamuua hawa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM hawampi credit ya kutosha Jumbe lakini ndiye aliyekuwa mtu wa mmuhumu sana nambari moja katika uundwaji wa CCM. Hamad alikuwa mtu mwenye tamaa ya madaraka siku zote za maisha yake na matokeo yake yalikuwa ni kuwafarakanisha Jumbe na Nyerere akitegemea kuwa ndiye angeweza kujaza nafasi ya Jumbe.!!
Jumbe alifanya mengi kwa Zanzibar na kama unakumbuka ndiye alikuwa wa kwanza kununua ndege ya rais wakati ule. Ukiwa kiongozi wa juu lazima uone haki inatendeka, huyu Hamad tamaa zake ndio zilizomponza. Hadi hivi leo nafikiri anajutia yale aliyoyafanya.
 
..naelewa nafasi ya Mwalimu Nyerere, na Mwalimu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

..kwanini unadhani Kawawa, Msekwa, na Thabit Kombo, walikuwa muhimu pia?
Jumbe alijua yeye ndo atamrithi Nyerere,alipokuja kugundua ilukuwa wakati wa kiroboto tapes na ikawa ameishachelewa.
 
..hizo ni siasa chafu baina ya wana-ccm.

..nyerere alilia machozi wakati akielezea jinsi kawawa alivyobebeshwa lawama ambazo alistahili yeye nyerere, au chama na serikali kwa ujumla.
Watu wa CCM kulia ni kawaida yao
 
Mkuu nadhani viongozi walioasisi TANU ndio wa kuenziwa, hawa wa CCM ni ''amalgamation''.

Kiongozi kama Msekwa anaenziwa kwa lipi? Huyu ametuachia mfumo hovyo sana wa Bunge.
Ni yeye aliandika miongozo mingi ya kulifanya Bunge lisiwe na meno na kuwa rubber stamp kama ilivyo leo.

Kosa kubwa tunalofanya ni kuangalia wanasiasa.
Siku za nyuma tulikuwa na sherehe za Mashujaa ambazo kwa hakika zilibeba maana yake halisi.

Tarehe ikaondolewa Sept 1, siku hizi hata kuwakumbuka waliojitoa kwa nchi hii kama wale waliolala Bunazi hakuna! Hatuwaenzi akina Kanal Kashmir, akina Walden, Mayunga, n.k.

Lazima kwanza tuwatambue wale walio ' pay the ultimate price''
Sethi Banjamin maskini.
 
Kuhusu siku ya mashujaa wewe unazungumzia mambo ta kitaifa, mimi nazuingumza CCM kama taasisi ya kisiasa kama ilivyo CHADEMA, UDP na vyama vingine. CCM inatokana na muungano wa TANU na ASP(ingawa hukuitaja); CCM isingekuwapeo kama vyama hivyo visingekubali kuuangana. Hao watu watano niolowataja ndio nguzo kubwa sana iliyofanikisha muungano wa vyama hivyo, na hivyo kuzaliwa CCM.

Iwapo Msekwa kama spika alivuruga, bado haimondolei credit kuwa wakati akiwa Katibu Mtendaji wa TANU alifanikisha muungano wa TANU na ASP na hivyo kuzaliwa kwa CCM. Hata hivyo utendaji wa Msekwa kama spika pia sikubaliani nawe kwa kiasis fulani, kwani Msekwa alikuwa ndiye spika wa kwanza kuongoza bunge lenye wabunge wa upinzani na aliwa-accomodate sana mpaka kukubali kiapo cha ubunge pia kibadilishwe.

Mwisho ni kwamba historia hujengwa na watu; wawe wanasiasa, askari au wanasayansi na kadhalika. Unaweza usimkubali mtu lakini akawa ni nguzo ya historia isiyoweza kubadilika. Mpaka leo sote tunajua kuwa aliyeanzisha vita ya pili ya dunia ni Hitller hata kama hatukubalini kabisa na itikadi yake lakini hatuwezi kubadilisha ukweli huo.
Umempiga chenga Kama ya Redondo
 
Watu watano muhimu sana katika historia ya uasisi wa CCM ni hawa:
1: Mwalimu Julius K. Nyerere
2: Sheikh Aboud Jumbe
3: Sheikh Rashid M. Kawawa
4: Sheikh Thabit Kombo
5: Mhe. Pius Msekwa

Inabidi CCM iwe na utaratibu wa kuwaenzi watu hawa kama waasisi wa taasisis yao.
Sio ccm ya Magufuli, labda ccm mpya baada ya Jiwe
 
Back
Top Bottom