Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 5,503
- 15,858
Tulipopata uhuru, matumaini yalikuwa makubwa. Tulidhani uhuru ungeleta maendeleo, uchumi imara, na maisha bora kwa wote. Lakini leo, Afrika bado inakabiliwa na umasikini, madeni, ukosefu wa ajira, na miundombinu duni. waasisi wa uhuru kama Julius Nyerere (Tanzania), Kwame Nkrumah (Ghana), na Jomo Kenyatta (Kenya) walituacha kwenye lindi la umasikini kwa maamuzi yao mabaya.
1. Julius Nyerere: Ujamaa na Kujitegemea au Umaskini na Madeni?
Nyerere alikuwa na ndoto ya kujenga taifa la usawa kupitia sera ya Ujamaa na kujitegemea lakini mambo yalikaa hovyo.
Alilazimisha watu kuhamia vijiji vya ujamaa kwa nguvu, akiharibu kilimo na uzalishaji.
Alinationalize viwanda na biashara, akiuwa sekta binafsi na kusababisha uhaba wa bidhaa.
Tanzania iligeuka taifa la ombaomba, ikitegemea misaada ya nje huku wananchi wakihangaika kwa umasikini.
Matokeo yake, Tanzania ikawa moja ya nchi maskini zaidi duniani, huku viongozi wachache wakifaidi mfumo uliokuwa unawaumiza wananchi.
2. Kwame Nkrumah: Baba wa Ujamaa na Madeni ya Ghana
Nkrumah alionekana kuwa shujaa wa Afrika, lakini alifanya makosa makubwa ya kiuchumi:
Alipuuza sekta binafsi na kuifanya serikali iwe kila kitu, hali iliyosababisha ufisadi na ukosefu wa uzalishaji.
Alikopa fedha nyingi kutoka nje ili kufadhili miradi mikubwa ambayo haikuleta tija.
Mwisho wa utawala wake, Ghana ilikuwa imefilisika na wanajeshi walimwondoa madarakani kwa sababu ya sera zake mbovu.
Leo hii, Ghana bado inapambana na athari za sera zake—madeni na umasikini wa kutisha.
3. Jomo Kenyatta: Uhuru kwa Wanawe, Umaskini kwa Wananchi
Kenyatta alionekana kuwa mwokozi wa Kenya baada ya uhuru, lakini aligeuka kuwa kiongozi wa matabaka.
Alijilimbikizia ardhi na mali huku Wakenya wengi wakiendelea kuwa maskini.
Aliacha ukoloni wa kiuchumi uendelee, huku makampuni ya wazungu na viongozi wachache wa Kiafrika wakineemeka.
Rushwa na ukabila vilianza kuwa sehemu ya utawala wake, hali iliyoweka msingi wa matatizo ya kiuchumi na kisiasa nchini Kenya.
Leo hii, Kenya bado inapambana na ukosefu wa ardhi kwa wananchi wa kawaida, ufisadi, na madeni makubwa.
Hitimisho: Wao Walipata Uhuru, Sisi Tulipata Umaskini
Waasisi wa uhuru walitufanya tuamini kuwa tumepata uhuru wa kweli, lakini badala yake walitufanya maskini. Walichukua nafasi za wakoloni, wakaendeleza ukiritimba wa kiuchumi, na wakafanya maamuzi mabaya ya kiuchumi ambayo bado tunalipa gharama zake.