Waathirika ghorofa lililoporomoka Kariakoo wafungua kesi mahakamani kudai fidia

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Waliokuwa wafanyabiashara ambao walipanga kwenye jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2024 wamefungua kesi kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania (Division ya Ardhi) Dar es Salaam wakidai fidia kwa waliokuwa wamiliki wa jengo hilo, ambapo madai ya fidia hiyo yanakuja kufuatia athari walizozipata kutokana na ajali hiyo ikiwemo upotevu wa mali na upotevu wa maisha kwa baadhi ya wenzao

Kesi hiyo ya ardhi namba 6075 ya mwaka 2025 inatajwa leo, Jumanne Aprili 29.2025 Mahakamani hapo chini ya Jaji Mohamedi Gwae

Kama mwenye jengo Hadi Leo hajulikani na wala hajashtakiwa hawa jamaa watapata Msaada gani?
 
Na wewe kabisa unaamini jengo halina mwenyewe?

Ni Tanzania tu unaweza kuokota vichwa vya treni bandarini, na kuokota gari Noah Tegeta.

Waliofunguwa kesi hawawezi kufunguwa kesi bila kuwepo mlalamikiwa.

Complainant vs Defendant, hapa lazima yawepo majina ya pande zote mbili au kampuni zao.
 
Aliyekuwa anapokea kodi ndiye tutaanza nae.
Huna logic, unaweza kupangishwa na kishoka tu.

Hapa tunadeal na fact na hivi ndio vitu vya kujifunza tusifanye mambo kienyeji.

Ndio maana mtu ananunua kwa mtu haki ya kuwa mpangaji wa NHC kwa pesa nyingi anakwenda NHC linawekwa jina lake badala ya kukaa sehemu unamlipa mtu badala ya kulipa shirika uwe mpangaji unayetambuliwa na NHC.
 
Na wewe kabisa unaamini jengo halina mwenyewe?

Ni Tanzania tu unaweza kuokota vichwa vya treni bandarini, na kuokota gari Noah Tegeta.

Waliofunguwa kesi hawawezi kufunguwa kesi bila kuwepo mlalamikiwa.

Complainant vs Defendant, hapa lazima yawepo majina ya pande zote mbili au kampuni zao.
Acha tusubiri tuone itakuaje
 
Huna logic, unaweza kupangishwa na kishoka tu.

Hapa tunadeal na fact na hivi ndio vitu vya kujifunza tusifanye mambo kienyeji.

Ndio maana mtu ananunua kwa mtu haki ya kuwa mpangaji wa NHC kwa pesa nyingi anakwenda NHC linawekwa jina lake badala ya kukaa sehemu unamlipa mtu badala ya kulipa shirika uwe mpangaji unayetambuliwa na NHC.
Naona umekurupuka tu kunijibu. Unajua utaratibu uliokua unatumika kwenye hiyo ghorofa? Unajua makato na kodi ya majengo zinavyolipwa?
Acha shobo na kujifanya kimbelembele.
 
Kwa nini usieleze hapa huo utaratibu badala ya kukata viuno tu?
 
Back
Top Bottom