Wababa awaangushia Diamond na Ney Wa Mitego tuhuma za wizi wa nyimbo zake

Wababa awaangushia Diamond na Ney Wa Mitego tuhuma za wizi wa nyimbo zake

sajosojo

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2010
Posts
1,021
Reaction score
636
Malalamiko ya wasanii kuibiana au kupigana kanzu kwenye kazi zao yaliripotiwa sana mwaka jana na mwaka huu mambo yalikuwa shwari, lakini baada ya kuvuka nusu ya mwaka yameibuka tena. Mshiriki wa shindano la kuimba la Bongo Star Search (BSS) , Wababa amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki
Gani' Nay wa Mitego na Diamond Platinumz kwa kumuibia kazi zake kwa wakati tofauti.

Akiongea kupitia Friday Night Live ya East Africa TV, Wababa amesema Diamond amemuibia wimbo wake ambao alikua anaiita ‘Kitorondo' na kwamba aliibadilisha jina baadae. "Kiukweli kuhusu Diamond, mimi mwenyewe nimetumiwa hiyo ngoma ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi ilivyo kuanzia idea, mwendo, style ambazo anafanya. Ambayo ameibadilisha jina tu baada ya ya kwamba ilikuwa mitandaoni nilikuwa nimemfatilia ilikuwa inaitwa Kitorondo mwezi mmoja kama uliopita. Kwa hiyo nilishindwa kulalamika kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa analalamika kuwa imevuja. Kwa hiyo sikuona
sababu ya kuongea kitu kwa sababu haikuwa official.

Kwa hiyo sikuwa na sababu ya kucomplaini kwa sababu haikuwa official, lakini mpaka jana ina maana ilikuwa serious kama biashara." Ameeleza
Wababa. Alipoulizwa ni wapi ambapo Diamond aliusikia wimbo huo, amesema huo ni wimbo wake alioutoa miaka minne iliyopita akiwa na Dogo Asley na aliuweka kwenye mtandao wakati anatumia jina la Nurdi, kabla hajaanza kutumia jina la Wababa aliposhiriki BSS. "Ni nyimbo ambayo iko mtaani na watu
wengi wanaielewa. Kwa hiyo sijaelewa.."

Kwa upande mwingine, Wababa amedai kuwa alifanya kazi na Nay wa Mitego katika studio za Mazoo lakini baaadae Nay alirudi studio na kuongea na Mazoo kutaka kuunua wimbo huo kwa shilingi milioni moja bila kumshirikisha Wababa. "Hivi karibuni nimefanya ngoma mpya na Nay wa Mitego, ni ngoma ambayo ilikuwa iko paid kwake pamoja na studio. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba siku mbili baada ya kufanya kazi nikapigiwa simu na producer akaniambia kwamba jamaa amerudi tena kwa ajili ya kutaka kununua wimbo kwa milioni moja, auchukue wimbo aende akaufanye sehemu nyingine. Baada ya hapo hata mahusiano yangu na mshikaji yamekuwa sio mazuri. Ukimpigia simu anakwambia yuko busy kuna kazi anafanya atanicheki, hadi kufikia leo sielewi ." Nay alipigiwa simu lakini hakuwa anapatikana kwa muda huo.
 
Heheeeee... Utachokaje ukija kusikia kwamba huyu jamaa kalipwa na diamond kutengeneza hizi tuhuma??????
Sina hamu na skendo za bongo.
 
Heheeeee... Utachokaje ukija kusikia kwamba huyu jamaa kalipwa na diamond kutengeneza hizi tuhuma??????
Sina hamu na skendo za bongo.

but uneuona huo wimbo wake huyu jamaa
 
but uneuona huo wimbo wake huyu jamaa

Wimbo wake sijauona wala kuusikia.. Wanaweza pia kuutengeneza kama ilivyokuwa kwa Daina kuupa promo wimbo mpya wa diamond.. Miaka minne wimbo upo upo tuuuuuu... Hahaaa
 
Ndo nimeusikia now.. The only similarity I have got is the name kitorondo ..
Huyo wababa si mzima kabisa, kwa hiyo ana hati miliki ya neno kitorondo?
 
Back
Top Bottom