Wababa wanalalamika sana kutengwa na watoto wao kimawasliano hata kiuchumi. Je, shida ni nini? Wamama mnaliongeleaje hili? Watoto mnafanya haya kweli?

Tatizo sio kubeba nafasi zetu. Wamama wanajua ku manipulate akili za watoto sana akipata ata kaupenyo kidogo jua umepigwa
 
Mwanaume lazima uwe na akili kuzid hawa viumbe katika vitabu vitakatifu wanasema tuishi nao kwa akili wanapokuwa mabinti hadi wakizeeka sasa ukimpa akili akushikie atakuonyesha kweli ye ni nani.
 
Sad[emoji26][emoji26]
Hata asipolalamika baba Mungu atamlalamikia
Ameamua kutuliza manyanga tu chini ndio amekuwa best wangu mbaya,sometimes anakuja hapa saloon kwang naamua tu kumnyoa buree tu
 
Huyo mzee aliwalea vipi hao watoto?
 
Huyo mzee aliwalea vipi hao watoto?
Hata kama aliwalea vibaya, huwezi lipa ubaya kwa mzazi wako

Hata wazazi wa kike nao wanayo mapungufu ila ya baba ndio wanaona kuwa hayawezi kusameheka sababu ni baba
 
Hata kama aliwalea vibaya,huwezi lipa ubaya kwa mzazi wako

Hata wazazi wa kike nao wanayo mapungufu ila ya baba ndio wanaona kuwa hayawezi kusameheka sababu ni baba

Hata kama aliwalea vibaya,huwezi lipa ubaya kwa mzazi wako

Hata wazazi wa kike nao wanayo mapungufu ila ya baba ndio wanaona kuwa hayawezi kusameheka sababu ni baba
We jibu swali uliloulizwa. Hayo mambo ya kufikirika achana nayo.
 
Ukweli unaouma!!!!
Kwanini hii ni zaidi kwa wababa kiafrika na sio Asia au Europe?
Ni kwasababu ya mentality, tamaduni zetu na gender roles zilivyogawanywa.Inabidi kubadilishe jinsi tunavyolea watoto,yale majukumu ambayo yalikuwa ya mama tu inabidi baba achangie pia katika makuzi ya mtoto kama kubadili diaper,kulisha,kuogesha,kuhudumia akiwa mgonjwa n.k
 
kwa kifupi usitegemee furaha yako itoke kwa mwanadamu ukifanya hivyo utajuta,ukitegemea watoto waje wakupe furaha nadhani utaishia kuwalaumu sana na hata kuwaingilia kwenye mambo yao ,hao wamama wanaopendana na watoto wao ndio chanzo kikuu leo hii ndoa nyingi kuvunjika utasikia " akikusumbua rudi nyumbani tu achana nae" au " kwani mwanamke yupo peke yake" ila wababa ni mara chache sana kusikia wanahusiswa na migogoro ya ndoa za watoto wao mara nyingi hukuta mama ndie anaeshitakiwa. Pia sishauri sana mtoto kuwa mtoto wa mama kila kitu mama pia wajaribu kumkumbuka baba katika mambo ya hapa na pale.
 
Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka don't expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
 
Wamama wengi hutumia muda mwingi na rasilimali zao kufanya uchochezi kwa watoto dhidi ya baba yao.

Watoto hupandikizwa chuki hasa wanapokuwa vijana wa kuanzia miaka kumi na kuendelea na kwa vile uwezo wao wa kudadavua mambo huwa bado mdogo huamini kile wanacholishwa na mama zao. Pili mtoto akikosa mama hukwepa kumuadhibu na humchongea mtoto kisirisiri kwa baba ili aadhibiwe kwa lengo la kumrekebisha na baba anatekekeza wajibu huo ambapo kama sio mama kuona kosa na kulisema baba asingejua wala kuadhibu. Adhabu hizo nazo huchangia baba kuchukiwa.

Tatu, wamama wengi hugoma kuchangia uendeshaji wa gharana za familia na kumuachia baba, kwa kuwa kipato cha baba ni kidogo wakati mwingine standard ya chakula au huduma zingine huwa za kiwango cha chini, hapo ndipo mama anapojifanya anawapenda na kuwajali watoto kwa kujitokeza na kutumia hela yake ambayo haitumiki katika bajeti kuu ya familia mfano siku hiyo inaweza kuwa imepikwa maharage lakini mama ananunua soseji na matunda au kuku na kuwaletea watoto, au mama kwa kuwa ana hela anawanunulia wanaye simu za bei mbaya. Kumbuka shule za boarding zote zinakataza simu lakini watoto huwa wanakamatwa na simu na mnunuzi wa hizo simu siku zote huwa ni mama.

Njia mojawapo ya kupunguza hili tatizo ni kuhakikisha pesa ya mama nayo inatumika katija bajeti kuu ya familia ili kupunguza pesa anayobaki nayo ambayo ndiyo anayoutumia kuwarubuni kuwa anawapenda zaidi kwa kuwanunulia vitu ambavyo baba hawezi au kumaadili anaona vitawapoteza watoto.

Lingine, inawezekana hawa wababa wanaolia leo kuhusu watoto wao nao waliwafanyia hivyo hivyo baba zao na sasa wanalipia maovu yao maana biblia iko wazi kuhusu hili: ukimheshimu mzazi wako na wewe utawafurahia watoto wako kinyume chake sahau.
 
Hapa kuna mambo mengi sana ya kuangalia

1.bond kati ya mtoto na mama ni kubwa sana kwa sababu ya shughuli za malezi ambazo kwa kiasi kukubwa zinafanywa na mama, mfano kuanzia kumuogesha mtoto, kumlisha, kuwapeleka shuleni na kuwasimamia homework jioni, wakati mwingine watoto mpaka wanalala baba hajarudi nyumbani

2.huu ukaribu wa mama na mtoto unamfanya mtoto anakua huru kueleza shida yake au mahitaji yake kwa mama, wakati mwingine baba ameacha pesa ya matumizi lakini mtekelezaji ni mama, mtoto yeye hajui kama pesa imaechwa na baba bali anajua my mom does everything for me, ndio pale unasikia mama anapambana ili tupate kila tunachokitaka

3.katika makuzi ya mtoto, baba muda mwingi yupo busy anatafuta, mama yeye anacheza na watoto, na kuwafundisha hata baadhi ya kazi na maisha ya kila siku, mtoto anapoumwa mama yeye yupo bega kwa bega, hii inatengeneza attachment kubwa kati ya mtoto na mama, mindset ya mtoto inakua ikitambua kwamba mama was always there for me

Kitu ambaco hawa baba zetu, au waume zetu hawatambui, ni kwamba mtoto anahitaji sana muda wa mzazi kuliko kitu chochote

Tunajua mpo busy kutafuta kwa ajili ya familia zenu, lakini mjitahidi mtenge muda wa kukaa na watoto na kuwafundisha mawili matatu, wakati mwingine hata kuwafanyia mambo madogo madogo kama kuwalisha/kuwaogesha, kufanya nao homework au kazi za hapa na pale once in a while, hii itasaidia kujenga bond kati ya watoto na baba zao
 
Siku hizi ni 50-50, baba na mama wote wanatoka alfajiri wanarudi magharibi. Jukumu la kukaa na watoto tumewaachia housemaids hivyo hakuna tena sababu ya baba kuchukiwa na watoto, unless awe kauzu.
 
Mimi nafikiri kitu kikubwa ni wazazi was kiume kuangalia familia lakini wasisahau kujiwekee aset zao Ili kama watoto watamtenga aset yake iweze kumsaidia maana unaweza kujali wanao lakini wasikujali ukiwa mtu mzima

Sent from my ONEPLUS A3003 using JamiiForums mobile app
 
Hata kama aliwalea vibaya,huwezi lipa ubaya kwa mzazi wako

Hata wazazi wa kike nao wanayo mapungufu ila ya baba ndio wanaona kuwa hayawezi kusameheka sababu ni baba
Ila pamoja na yote, madingi wenu miyeyusho tena sana.
 
Siku hizi ni 50-50, baba na mama wote wanatoka alfajiri wanarudi magharibi. Jukumu la kukaa na watoto tumewaachia housemaids hivyo hakuna tena sababu ya baba kuchukiwa na watoto, unless awe kauzu.
Unajizungumzia wewe au jamii nzima?Hata kama watu wanafanya kazi 50-50 bado wanatakiwa kusaidiana majukumu wakiwa nyumbani ya malezi so haibadilishi fact ya kwamba wababa waliowengi wanakitoka kazini wanaishia bar au wanakojua wao na mama ndo anabeba mzigo wa ulezi!
 
Mtoto kalelewa na dada wa kazi na movie za Mnet series ataanzaje kumpenda baba yake uzeeni wakati amefunzwa na movie
 
Ameamua kutuliza manyanga tu chini ndio amekuwa best wangu mbaya,sometimes anakuja hapa saloon kwang naamua tu kumnyoa buree tu
Mungu ampe amani
 
Mtoto kalelewa na dada wa kazi na movie za Mnet series ataanzaje kumpenda baba yake uzeeni wakati amefunzwa na movie

Hata waliolelewa bila dada wa kazi na movie wanafanya hayohayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…