Tabia mbovu kwenye jamii zimekuwepo toka enzi na enzi. Incest imekuwepo japo inafichwa.Jamii nyingine kwa kuona kuna practice kama hiyo wamehalalisha kuoana mabinamu/first cousins. Siyo baba tu wenye tabia hizi, wapo kaka na dada, mama na mtoto wa kiume ( japo ni nadra sana.. nimewahi kusikia kesi moja tu yenye uhakika ukiacha rumours)...
Tukirudi kwenye hili la baba na binti, kinachotokea ni ama ushirikina au baba kujiendekeza kwenye tamaa za kimwili na kushindwa kujizuia.Pia mabinti nao wengine hawajiheshimu mbele ya baba zao. Hujiweka kihasara na kuvutia hisia na tamaa mbaya kwa mzazi wa kiume.Ndio maana jamii nyingine mtoto wa kike akishapevuka haruhusiwi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na baba.Kila kitu kinapitia kwa mama! Siku hizi malezi yako huria zaidi. Baba na binti hucheza rhumba kwa kukumbatiana kwenye mziki, baba na binti huketi sebuleni kuangalia "Shades of Sins" na tamthiliya nyingine - shetani naye hufanya kazi yake barabara!Pamoja na yote hayo, bado hatumpi baba kibali cha kujiendekeza!