olimpio
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 418
- 866
Katika kipindi hiki ambacho dunia inageuka kutoka analogy kwenda digital, utendaji wa sekta binafsi na serikali vinabadirika kwa kasi sana.
Leo tuwaangalie wachache kati ya wengi, viongozi wanaoongoza mageuzi ya kidigitali nchini, toka sekta binafsi na sekta ya Umma.
1. Vodacom Managing Director (Philip Besimire)
Huyu hana muda mrefu toka ajiunge na Vodacom, lakini kabla ya kujiunga na Vodacom alikua kampuni moja ya simu ya South Africa inaitwa MTN.
Vodacom, kama moja ya kampuni ambayo imejipambanua kwa matumizi ya TEHAMA na mifumo ya kisasa kabisa, inaongozwa na kijana huyu Mganda kwa utaifa wake. Vodacom si tu wamekua wa kwanza kuleta 5G nchini bali wanayo slogan yao ya yajayo yanafurahisha, yajayo ya kidigitali, ukiacha bundle zao kuwa za gharama Vodacom ni moja ya kampuni bora sana zinazo promote uchumi wa kidigitali.
2. Mkurugenzi Mkuu wa TCRA ( Dr Jabiri Kuwe)
Huyu Dr wa chuo kwa vigezo vya kielimu, Amehusika kwenye mbio za mwanzo kabisa za UCC pale UDSM, akaenda kuwa Mkurugenzi wa kwanza wa EGA (Serikali mtandao) kwa zaidi ya miaka 8 na kuwezesha mifumo karibu yote inayotumika serikalini kutengenezwa tena na vijana watanzania pale EGA, na sasa nimkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).
Huyu ni chuma kweli kweli amefanya mageuzi makubwa ya mifumo ya TEHAMA akiwa EGA na sasa TCRA baada ya kuhamishiwa hapo, inasemekana Ameifanya TCRA kuwa moja ya taasisi bora sana kwa matumizi ya TEHAMA nchini.
3. Mkurugenzi Mkuu wa TIGO Mapaka 2021 sasa yupo Msumbiji kama CEO WA Vodacom huko (Simon Karikari).
Huyu mwamba amekua mkurugenzi mkuu wa Tigo kwa zaidi ya Maika 7, ameiwezesha Tigo si tu kuwa moja ya kampuni bora kabisa lakini kuwa kampuni inayo stimulate digital transformation nchini. Ikumbukwe Tigo ni moja ya kampuni kubwa mbili nchini ukiacha Vodacom, na Airtel kwa mbali kidogo.
4. Gavana wa BOT (Emmanuel Tutuba)
Chuma hiki toka kuwa RAS Mwanza, katibu mkuu wizara ya fedha na mipango , mpaka Gavana wa Benki yetu kuu, kwa muda mfupi amabo amekuwa pale BOT anaongoza mageuzi makubwa ya uchumi wa kidigitali, CRYPTO CURRENCY ni moja ya agenda yake kuu ambayo soon tutasikia BOT inaleta mwongozo wa kuregulate hii currency ya kidigital,
5. Mkurugenzi mkuu EGA/Serikali Mtandao (Eng. Benedict Benny Ndomba)
Huyu Mhandisi amerithi mikoba ya Dr Jabiri, mwanzo hakuna walioamini kama anaweza kuvivaa viatu vya Dr. Jabiri, kwa sasa EGA inaongoza nchi kuing'arisha kidigitali, siku chache zilizopita, serikali ilitangaza kuwa Bank ya dunia imeiweka Tanzania kama nchi ya 2 AFRIKA kwa matumizi sahihi ya TEHAMA serikalini, kwenye string ni Ndomba, na mtangulizi wake Bakari aliyeweka misingi kwa zaidi ya miaka 8.
6. Waziri, Wizara ya TEHAMA (Nape Nnauye)
Katika mawaziri wachache sana ambazo wameweza kuituliza wizara yenye jukumu la kuiongoza nchi kidigital ni Nape, huyu mwanasiasa ana weledi wa kipekee sana, anatoa nafasi kwa wataalamu wa technolojia kufanya kazi zao bila kuwaingilia, anapokea ushauri na hapendi siasa kwenye TEHAMA. Mabadiriko makubwa kwenye wizara ya TEHAMA na mpaka nchi iko kidedea kwa matumizi ya TEHAMA waziri Nape ana mkono wake.
7. Mkurugenzi wa Idara ya IT, Wizara ya Fedha na Mipango (John Sausi)
Mkisikia GEPG, hio ni moja ya project alizozisimamia huyu mkurugenzi, Malipo kupitia Control number ni project ambayo kamwe haiwezi kusahaulika, mradi huu mkubwa ambao John Sausi ameusimamia pamoja na mkurugenzi wa EGA wa kipindi cha nyuma Jabiri Kuwe ni wa mfano na wa kipekee sana. makusanyo ya mapato ya nchi yapo kidigitali sasa, hadi vijijini wanajua control number, john Sausi alihusika kutekeleza maono haya ya wakuu wa nchi.
=============================================================================
Hawa ni wachache kati ya wengi amabo Tanzania inajivunia kuwa nao hasa kwenye kipindi hiki cha kidigitali.
Rais wa nchi hii akiendelea kuwatumia vyema watu hawa Tanzania kidigital itapaa sana.
Unaweza kuongeza na wengine tuwape maua yao.