BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki amesema watumishi 116 wamechukuliwa hatua kutokana na ubadhirifu fedha za umma.
Kairuki ameyasema hayo Jumamosi Novemba 5,2022 wakati akichangia taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali, (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).
Amesema hadi kufikia Agosti, 2022 watumishi 116 walichukuliwa hatua kutokana na ubadhirifu.
Pia amesema wameelekeza ofisi za makatibu tawala na wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa Novemba 15, mwaka huu wanapeleka awamu ya pili ya watumishi waliochukuliwa hatua.
“Ukiangalia tuna watumishi zaidi ya 22 wameshafikishwa mahakamani, kuna watumishi zaidi ya 23 wameshafikishwa TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa),”amesema.
Amesema watumishi watatu walifukuzwa kazi, 20 wamesimamishwa, watumishi 47 wamepewa onyo na mtumishi mmoja ameshushwa cheo.
Amesema watumishi 57 wameshushwa vyeo pamoja na kuwavua vyeo waweka hazina 15, wakuu wa idara zaidi ya 14, maofisa mipango watatu, wakuu wa vitengo vya wakaguzi watatu na kuhamisha watumishi 384.
MWANANCHI