Wabakaji sasa wamekuwa Mapadre, Masheikh, Wachungaji na Wazazi

Wabakaji sasa wamekuwa Mapadre, Masheikh, Wachungaji na Wazazi

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Kuna li mtu ni libakaji ,ni linajisi...limeamua kuwa Sheikh. Limeamua kuwa Padre, Limeamua kuwa Mchungaji na Lingine limeamua kuwa Baba.

Limeamua haya yote huku lina akili ile ile ya kubaka, kulawiti na kunajisi.

Usihukumu Dini. Angalia Dini inasemaje suala la mtu mzima kutembea na mtoto ambaye ni mdogo anapaswa awe mtoto wake. Hapo ndo ungeweza laumu. Lakini kama Dini zinakataza then sidhani ni vyema kuwasema Wakristo , Waislamu, Wahindu, Waasili.

Je, Dini zao zinawapa aya za wao kulawiti? Kubaka? Kunajisi? Kusodomize? Mijitu hii ya ovyo inapata nafasi ambazo inazitumia kumfurahisha shetani.
 
Majitu yanayoaminiwa na jamii ndo yamekuwa mwiba mkubwa kwenye maisha ya watoto na baadhi ya watu wazima....!
Wengi ni vichaa waliopewa nafasi na jamii na kuaminiwa..... Afya ya akili !!!
 
Kwa kweli ni vitendo vinavyosikitisha sana hasa pale vitendo hivyo vinapofanywa na watu walioaminiwa na jamii

Sasa tukimbilie wapi?

Juzi tulikuwa tunajadiliana na jamaangu fulani hata majibu hatukupata wote tulibaki hatuewi.

Matukio yamekuwa mengi ya kikatili na ya kutisha hatari

Inakuaje Padre, mchungaji nk, wanafanya matendo ya namna hii!
 
Mm nasemwa sana vibaya kibaruani, na watumishi wa bwana. Hawakosi ibada, nikajua kuna shida sehemu
 
Sikumbuki hata mwisho lini kwenda kanisani kwa sababu mara ya mwisho kwenda niliona utapeli kwa njia ya biblia nikasema nitaishi kwa neno bila kukanyaga kanisani

Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Bwana
Upako ninaopata from hii hillsong gosple
Naamini he will make a way
 
Back
Top Bottom