Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wabantu walisambaa kutoka maeneo ya Cameroon na kuelekea kusini yote ya Africa kama miaka 3,000 iliyopita, yaani miaka 1000 kabla ya kuzaliwa Yesu. Lakini kabla ya wabantu kuja huku kusini, wakazi wa asili wa huku walikuwa nani?
Huku kulikaliwa na mbilikimo, wabushmen(San) kama wakhosa wa South Africa na Wasandawe na wahadzabe wa Tanzania. Pia kwa Africa mashariki kama Tanzania, wakush wa kusini kama wa Iraqw tayari walikuwepo.
Ilichukua miaka mingi sana kwa wabantu kusambaa huko kote. Njiani mote, hasa kwenye misitu waliingiliana na mbilikimo na kuchangamana kisha jamii nzima ikaunga safari.
Kuchangamana huku ndiko kumefanya wabantu waliokuja huku kusini kuwa na upimbi-upimbi ukilinganisha na 'wabantu' walioenda Africa ya Magharibi. Wabantu wafupi ni mbilikimo waliokuwa assimilated kwenye ubantu.