sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,001
Wakuu heshima kwenu
Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikifatilia siasa za nchi zetu za Afrika mashariki hususani kipindi Cha uchaguzi.
Rwanda na Uganda sijashuhudia chaguzi zao hivyo naziacha Kama zilivyo kwanza.
Katika nchi zinazounda jumuiya ya Afrika mashariki,ni Kenya tu ambayo ukiangalia siasa zao unaweza ushindwe kujua kuwa wanaigiza ama wapo serious na wanachokifanya. Nakama wapo serious nchi majirani tuige mifumo yao au tuachane nao?
Kenya hakuna chama cha kisiasa chenye uhakika wa kutawala zaidi ya awamu mbili tangu ilivyoondoka KANU mwaka2002.
Kenya chama kinachompata raisi kinajifia mara tu utawala wa raisi husika unapokoma. Rejea kile chama kilichomuweka madarakani hayati Mwai Kibaki, na hata hiki kilichomuweka madarakani Uhuru Kenyatta.
Kenya hakuna kubebana kisiasa kwa kisingizio cha tupo wote serikalini.Hii inajidhihirisha pale ambapo raisi Uhuru alivyokuwa kinyume na makamu wake kwenye kampeni huku akionekana dhahiri kumpigia kampeni mzee Raila Odinga. Pia ikumbukwe Kuna mawaziri walijigawa mapema wengine wakaenda kambi ya William Ruto huku wengine wakiwa upande wa Hapa unashindwa kuelewa kwenye vikao vya baraza la mawaziri wanakaaje na kuelewana kwenye Mambo muhimu ya kitaifa.
Kenya wanachagua raisi wao hata wakiwa nje ya Kenya. Uchaguzi huu wakenya walioko mabara mbalimbali wamepiga kura kwenye balozi zao.
Uhuru Kenyatta aliamua kuachana na chama Cha baba yake ambacho ndio chama Cha ukombozi nchini Kenya(KANU).
Wakuu,hii yakuachana na chama Cha baba walau kidogo inaweza kufanana na Ile ya Makongoro wa Tanzania aliyehamia NCCR nakuachana na CCM ya baba yake (japo alirudi).
Ninachoamini nikwamba hata baada yauchaguzi huu wa Kenya,chama kitakachoingia madarakani hakiwezi tena kujitokeza baada ya mihula miwili ya uongozi wake kupita(Kama kikichaguliwa kwa mihula miwili).
NB: Kila hoja niliyoandika nimeilinganisha na nchi ya Tanzania.
Naomba kusaidiwa;huu mfumo wa siasa na chaguzi za Kenya,unawezwa na wakenya peke yao ama hata sisi watanzania tunaweza kwenda nao?
Wasalaam!
Kwa kuongezea; Wakenya hawapigi kura kwa kuangalia chama bali wanaangalia mtu, kwao chama baadae.Tofauti na nchi zingine ambazo chama chao kikishateua hata Kama ni boga litapigiwa kura za ndio.Ikibidi litasaidiwa kwa kuiba kura.
Kenya hawana vijana wanaoshinda na kukesha kwenye vibaraza vya ofisi za vyama vya siasa. Mambo ya vyama kwao yanasikika wakati wa uchaguzi tu.