Katika tathmini au uoni wako hapo ndo umeona vizuri, ila hujaona kwa undani.
Kenya kuna chama kimoja kikuu cha siasa. Chama hicho ni kabila na ukanda.
Ukanda wanaojiita "watu wa milimani" yaani wakikuyu na wakalenjini na wengineo wa maeneo ya Mlima Kenya ndiyo wanaotawala.
Asili ya hawa watu kutawala ni kwamba Mzungu anapenda sehemu za baridi kama vile Iringa na Mbeya. Kwa hiyo Mzungu alipovamia Kenya alikwenda moja kwa moja kukaa maeneo ya baridi na mji mkuu akaweka Nairobi ambako ni eneo la baridi.
Ili mzungu akae ilibidi awafukuze waAfrika waliokuwa wanaishi hapo, wengi wao wakiwa ni waKikuyu. Aliwafukuza halafu akachukua ardhi yao akalima kahawa, na ili waAfrika hao waje kumfanyia kazi kama manamba akatunga sheria ya kodi ya kichwa, ambayo usipolipa unaadhibiwa kwa kudhalilishwa kwa kuchapwa viboko hadharani eneo la sokoni, au mbele ya mke na watoto wako. Au ukiwa sugu zaidi unafungwa jela.
Kwa hiyo wale walioporwa ardhi wakajikuta tena wanalazimika kuwa watumwa kumlimia mzungu kahawa zake ili wapate pesa ya kulipa kodi. Maana pesa halali ilikuwa ni ile anayochapisha mzungu.
Hapa ndo watu wa milimani wakapata hasira mara kumi dhidi ya mzungu na kuhakikisha wanapigana naye kufa na kupona aondoke kwenye ardhi yao.
Mzungu kwa kutambua kuwa hawa watu aliowapora ardhi wanamchukia akaenda kwa wajaluo ambao ni watu wa bondeni kwenye ufukwe wa ziwa Nyaza ila aliowaona wana akili za darasani. Hawa ndo akawapa kipaumbele cha kuwasomesha elimu yake ili wamsaidie kazi za kiutawala ofisini. Hakutaka wakikuyu na wakalenjini ambao alikuwa amewapora ardhi wasome na kukaa maofisini maana wangemhujumu.
Wajaluo ni wapenda sifa sana, na kitendo cha kutunukiwa hadhi hiyo na Mzungu kikawavimbisha vichwa, wakajikuta wanafurahi kushiriki kwenye ukoloni.
Kitendo hiki kiliwachukiza sana wakikuyu na wakalenjini. Hivyo harakati zao za kudai uhuru zilipofanikiwa waliapa kwamba
Mjaluo hatakuja kutawala Kenya!
Hizo ndo siasa za Kenya. Hivyo vyama vinavyobadilika kila msimu wa uchaguzi visikusumbue. Na katu usije ukapiga debe kwamba Tanzania iige siasa za Kenya. Tuna urithi tofauti kidogo kati yetu na wao.
Wajaluo nao wana hasiria sana kwa sababu ya kuwekwa kando kwa miaka 59 sasa, kwa hiyo Uhuru Kenyatta ni kama aliona awahurumie kidogo. Aidha ni hivyo au ni mchezo tu wa kisiasa kwa sababu katika siasa mara nyingi sana mgombea anayeungwa mkono na Rais anayemaliza muda wake huwa anakataliwa na wapiga kura. Kwa hiyo kama wewe ni Rais ukitaka kumsaidia mgombea wakati mwingine ni vizuri ukampiga vita waziwazi ili wananchi wakuchukie wewe Rais unayeondoka na wamuunge mkono mgombea uliyesema humtaki.
Watu wa Pwani wao kwa kuona wametengwa katika hili bifu kuu la kati ya watu wa milimani dhidi ya wajaluo wao wakaona watangaza kujitenga. Walifanya kampeni na vuguvugu la
Pwani si Kenya mwaka 2010-2011 wakitangaza Jamhuri ya Mombasa kuwa ni jamhuri huru iliyojitenga kutoka kwenye Jamhuri ya Kenya. Hii ilitokana na vita iliyoibuka kati ya watu wa milimani na Wajaluo kufuatia uchaguzi wa Rais wa Kenya wa mwaka 2007 ambapo Wajaluo waliona mtu wao Raila Odinga amenyang'anywa ushindi.
View attachment 2320307 View attachment 2320312