Wabongo hizi chuki zinasababishwa na nini?

Wabongo hizi chuki zinasababishwa na nini?

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Utakuta umeenda ofisi flani kiofisi umekaa zako na kazi zako simu imeita umetoa iPhone 11 yako umeongea umemaliza unaskia kamjadala kaajabu watu wanaongeleshana “ yaani mimi nitoe milioni yangu ninunue simu? Kweli wabongo wanapenda matumizi unakuta mtu ana simu ya millioni tatu wakati maisha yake kama ya kwangu tu heheee” mwingine utamsikia “ wee mimi TECNO yangu nimenunua laki na nusu na ina miaka mitatu inapiga kazi yaani nitoe milioni ninunue simu hehehe”

Ukute uko zako kitaa kwenye ki glosari kuna majirani kadhaa wapo kivyao wanakunywa K-Vant umeagiza dompo lako basi utaskia vi mjadala vya ovyo kweli “unajua mimi hizi pombe tamu tamu siwezi kunywa kwanza zina sukari, alafu ogopa sana vitu vyenye rangi rangi sana sana hizi wine siyo nzuri kiafya” yaani ilimradi tuu wajiridhishe kuwa wao wako vizuri kimaamuzi kuliko wewe sijui hii tabia inasababishwa na nini wabongo kwanini msi mind mambo yenu bila kijilinganisha na wenzenu?
 
Mkuu umeua sisi wabongo bila maisha ya watu wengine hatujion kama tunaishi

Sisi watz bila umbea na unafiki tunaweza tusitoboe tutakufa kwa sonona
 
MKUU,
CHAGUA CHAUMA,
CHAGUA #HASHIMU_RUNGWE_SPUNDA ILI TULE WALI NA KUKU WA KIENYEJI BILA WASIWASI!!!
 
Hadi K vant nayo kuna watu wanaionea wivu?
Hama hiyo mitaa
 
Hapa watakuja wale wa stalert Vs Harrier
 
Hadi K vant nayo kuna watu wanaionea wivu?
Hama hiyo mitaa

Hata ukinywa valuu watakujadili ili mradi tuu wao wajione wanakunywa kitu chenye afya zaidi yako yaani ilimradi tuu waridhike wao ndiyo wako sahihi zaidi
 
Mkuu umeua sisi wabongo bila maisha ya watu wengine hatujion kama tunaishi

Sisi watz bila umbea na unafiki tunaweza tusitoboe tutakufa kwa sonona

Yaani ukikaa na gari lako watakujadili utaskia “ sasa gari miaka yote yuko nalo si auze tu afanye maendeleo”.
Ukisema uuze gari utaskia “gari ni gari bwana lina hadhi yake hata liwe baya vipi huwezi kufafanisha na asiye na gari, kweli maisha yanaenda yakibadilika leo anakula vumbi hehehe” yaani ilimradi tuu ujutie maamuzi yako.
 
Kwa hiyo umechagua upande wa IPhone na dompo ili ueleweke kwa urahs au sio..

Mkuu usisite kuntupia wawili watatu maporomoko ya PM yakianza..
 
Kwa lugha nyepesi isiyo na ukakasi Ni Kwamba.
Waswahili/watanzania tulio Wengi chuki tumetoka nazo tumboni .
Ziko kwenye DNA kabisa.
 
Lakini hata mimi siwezi kutoa 1m kununua simu. Sio kwamba nina wivu au chuki wewe kumiliki iPhone,hapana ndio ukweli wangu.
 
Back
Top Bottom