Watanzania kwa kweli tunaumizana kuliko watu wengine hapa duniani.ni kwamba kila utakacho nunua dukani ujue umeibiwa;kwa mfano ukinunua saruji ujue kuna kilo kama tano hivi mpaka nane hazipo,ukinunua nyama, sukari, unga, maharage.vyote kama ni rejareja ujue umeumia.haya siku hizi hata sabuni hizi za bongo za unga na vipande hazitoi povu kabisa utafikiri unafulia mbao,petrol ndio usiseme mafuta ya taa kibao,tunashindwa na vijinchi kama Rwanda Burundi hata Zambia wana sabuni nzuri sana,haya halafu hawaTBS sijui wanafanya nini maana wapo na wanaona sana wakisha toa aprove basi hata kucheki prodact inakuwa basi tena.ukinunua dawa ya meno utakuta hewa tupu kwenye tube,wajameni haya ni baadhi tu.nawasilisha hoja