Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Wabongo wa majuu hamna umoja mnajigawa

Kweli kabsa kuna matabaka sanaa wabongo wanoishi majuu- hakuna umojakabsa, majungu moto, wivu mwenzako akikuzidi kipato, tafarani na nafikiri hii haiwezi kuisha tafuta ambao mnaendana ishi nao hayo mengine hayawezekani kukaa sawa

Nipo hapa tu SA- sijafika hata huko LONDON lakini mfano nauona yaani watu wanatumiana hadi watu waende kumuua mwenzao au kumwagia hata tundikali

Yaani Mungu ajaalie tu ili bichi niliruke niende hata MAKANADA huku hapa pagumu sanaa ila najichanga nasikia ml10 tu naingia Kwa aunty ELIZABET-InshAAllah
 
Mkuu,

Inakuwaje watu wengine tukawa hatuwezi kabisa kuwa na chuki kwa mtu kwa sababu kafanikiwa, na wengine wanakuwa na chuki hivyo?

Binafsi nikiona mtu kapata mafanikio ninayoyataka, nafurahia mtu kafanikiwa, najiuliza na mimi nifanye nini nifanikiwe hivyo, najaribu kadiri ya uwezo wangu.

Nikifanikiwa nafurahi, najaribu kusaidia wengine kadiri ya uwezo wangu.

Nikijaribu sana kifanikiwa na kushindwa, nakubali hali yangu na kuridhika bila kumuwekea chuki aliyefanikiwa, nikijua kwamba ama sina uwezo unaotakiwa kufanikiwa hivyo, ama hata kama nina uwezo, mambo mengine ni ya bahati tu na unaweza kuwa na uwezo ukakosa bahati.

Tena nikiona mtu kafanikiwa kuliko mimi, napeleleza kanizidi nini ninachoweza kujifunza kutoka kwake, namuwekea heshima kwamba huyu kafanikiwa kuliko mimi, namuheshimu kwa hilo, kuna kitu naweza kujifunza kutoka kwake. Naangalia mapungufu yangu na jinsi gani naweza kuyapunguza kwa kutumia mfano wa huyu mtu. Nampenda kwa kuwa ananipa nafasi ya kujiongeza.

I almost don't want to be the smartest person in the room, because that means there will hardly be any growth for me in that room.

Kwa nini watu wengine wanashindwa ku focus kujiongeza wao wenyewe kujaribu, wafanikiwe, na hata wakishindwa kwa nini wanakuwa wagumu kukubali hali zao na kufurahia mafanikio ya wengine bila kinyongo?

Najaribu kuelewa hii chuki inatoka wapi.

Mimi nafikiri kwa aina fulani nina ego kubwa, kujiamini fulani mwenyewe kukubwa sana, nafikiri ninaweza kufanya mengi ninayotaka na kumchukia mtu kwa sababu ya mafanikio yake ni kama kukubali kwamba mimi siwezi kufanikiwa ninavyotaka.

Na watu wenye hii chuki ni watu fulani ambao wana walakininkatika kujiamini kuwa wanaweza kufanikiwa.
 
mkuu mjaribu member ainaitwa izzo lakini kwa sasa sioni akitoa michango
Ahsante mkuu ngoja nimcheki jamaa
Huyu mtu wako "Izzo" ni tapeli tu tulikuwa naye kwenye ile thread maalufu JF ya kujilipua kwenda mamtoni back in 2017. Akaleta mawenge. Kiufupi kama unataka kwenda mbele unapaswa upambane kivyako achaheni kulialia.

Kaveli
 
Kweli we mbongo 🤣🤣🤣
 
Dada mdogo wa Kiranga mbishi kuliko Kiranga

Anabishana mpaka na serikali ya Marekani!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hilo alilofanya ni kujiamini na kutokuwa mnyonge kitu anbacho ni zao la malezi bora toka utoto, suala ubishi ni wewe😂
 
Mkuu Kiranga wewe unahitaji ubatizo hapo ziwa michigan[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama nilivyosema chuki ni asili ya mwanadamu. Isipokuwa mazingira unayoishi na maarifa unayoendelea kuyapata kupitia life skills mbalimbali zinamchango mkubwa wa kubadili asili yako na kukufanya uwe kiumbe kingine kutokana na hayo mazingira uliyopo au maarifa unayoendelea kuyapata.

Kama nafsi yako inafurahia mafanikio ya watu wengine, basi wewe ni miongoni mwa watu wachache sana waliofanikiwa. Namanisha kufanikiwa kwa utajiri wa maarifa. Kama wewe ni miongoni, chunguza tu maarifa uliyoyapata kuanzia angalau miaka 10 huko iliyopita. Hali uliyonayo leo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazingira uliyojitengenezea kuanzia miaka mingi iliyopita.
 


Chillah
 
Inawezekana kuna ukweli mwingi kwenye maneno yako.

Nature yetu ni kushindana, mambo ya zero sum game kwenye game theory, yani tunaona ukipata wewe maana yake nimekosa mimi.

Wakati, ukweli inawezekana wewe upate na mimi nipate pia, yani iwe kwamba kuna cha kutosha kila mtu, ni jinsi tunavyojipanga tu.

Mimi nililelewa kwenye familia za kilokole, halafu nika hang sana na ma Rasta wale wa peace and love, halafu nikaenda Buddhist Temple nikasoma sana loving kindness ya Buddhism na kuwa rafiki sana na Buddhist monks, halafu nikasoma sana falsafa za humanism na jinsi watu wanavyoweza kujitengenezea maisha ya upendo.

Halafu nimekuja kugundua nimepata bahati bahati za kunirahisishia maisha, ila hata nilipokuwa na wakati mgumu nilikuwa na ujeuri fulani wa ku focus kwenye maisha yangu bila kinyongo na mtu. Yani nimeishi kama vile kinyongo na mtu aliyenizidi kinatumia energy yangu na kunitoa kwenye focus ya kujiongeza kwenye mambo yangu.

Kwa hivyo, kama ulivyosema, inawezekana hiyo safari yangu ya maisha imechangia kunifanya niwe mtu ambaye ni vigumu kuwa na kinyongo na mtu kwa sababu kanizidi kwenye mafanikio ninayoyataka.

Kama hata naweza kukubali kuwa kuna mtu aliyenizidi katika mafanikio ninayoyataka.

Yani nina uwezo mkubwa wa ku justify kwamba "hizi hela za Elon Musk hizi zingeniondolea faragha yangu, na mimi napenda faragha kuliko kuwa tajiri wa dunia, au zingeniua mapema tu, na mimi napenda kuishi".

Tayari nishaondoa sababu ya kumchukia Elon Musk kwa sababu ya utajiri wake

Tena ndiyo kwanza naanza kumuonea huruma [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
'US ya sasa sio kama ya zamani' -Maneno ya mwanandugu dayaspora.Tusubiri kuletewa simu zilizovuja wino,raba oversize na majaketi tu.Michongo kwa mbongo sahau roho mbaya sana .Halafu walivyo washenzi wakija wanakulazimisha upige picha huku umetabasamu.Natabasamu vipi huku hali mbali .Sitabasamu chochote.Stupid.
 
Mkuu,

Pole kwa uzoefu huo.Simaanishi kukanusha uzoefu wako binafsi.

Lakini, tukiondoka kwenye uzoefu binafsi ili tupate picha kubwa zaidi.

Kunakuja swali.

Kwani wabongo wote walio US wako sawa?
 
Mkuu,

Pole kwa uzoefu huo.Simaanishi kukanusha uzoefu wako binafsi.

Lakini, tukiondoka kwenye uzoefu binafsi ili tupate picha kubwa zaidi.

Kunakuja swali.

Kwani wabongo wote walio US wako sawa?
Hapana hawako sawa na samahani kwa kufanya generalization.
 
Mkuu ingia kichwa kichwa ule za uso
Huyo Dr kuna uzi humu jamaa alilalamika alitaka kumtapeli

Alijifanya anafanya kazi TRA anataka kumtaftia driving license akawa anamlazimisha amtumie laki 2

Ngoja ntafte ule uzi ntauleta hapa


Na huyu kiranga mi naamini yupo mbele na anajua vitu vingi sana, in short kwangu kiranga ni akili kubwaz,

But jamaa haamini uwepo wa Mungu, ogopa sana mtu haamini uwepo wa Mungu
 
Wewe unajiita mwalimu wa tuisheni,hivi unaakili timamu kweli?

Hivi walimu wote wangekuwa na akili kama zako tungesoma kweli?

Kwa kifupi wewe ni zezeta na kama unataka msaada kutoka kwa mumeo sema usiogope
Maticha most of them ni wajinga wajinga tu, just imagine wanazidiwa akili hata na mpwayungu village
 
Ndio Mkuu. Tunaweza kuhitimisha kwa kusema ni muhimu sana mtu kutafuta kujiongezea maarifa mengi zaidi kwenye haya maisha. Watu tusiishie kuwa na maarifa ya careers zetu pekee. Bali tutafute na maarifa mengine mengi yanayohusu maisha ya mwanadamu hapa duniani. Ukiangalia anachokilalamikia ndugu mleta mada ni matokeo ya watu kutokuwa na maarifa ya maisha. Usipokuwa na maarifa ndio utamchukia mtu, unakuwa mtu mwenye wivu, utaseng'enya sana, utakuwa muongo muongo, mpika majungu, mbabaishaji, usiyeaminika n.k.
Ni bahati mbaya sana kwamba watu wengi hawapendi kujiongezea maarifa.
 
Kote kote wanaangalia hivyo vitu kwenye suala la kwenda kuishi na mwenza ila (sijui kwa marekani) kwa nchi za Scandnavia ukishapata visa ya kwenda kuishi na mwenza wako sio kama ndio ushamalizana nao bali baada ya miaka miwili wewe na mwenza wako mtaitwa kwenye interview ya mwisho yenye lengo la kuwapatia permanent residence permit.
Na iwapo imetokea mmeachana kabla ya hiyo miaka miwili mgeni anaweza kurudishwa nchini kwao.
Hilo swali sio la kawaida na ndo mana nimelitumia kama mfano na walioulizwa hilo swali hawakupewa hiyo permit.

Wanaouliza hayo maswali wanacheza zaidi na saikolojia na kila swali wanalouliza wanakua na sbb ya kuliuliza na huwa hawazingatii majibu tu wanaangalia vitu vingi.
 
Mkuu,

Ogopa sana mtu anayeamini uwepo wa Mungu.

Nitakupa story moja.

Siku moja tulikuwa tunapiga story group la Whatsapp la shule.

Ghafla, mwenzetu mmoja akawa analalamila kuwa anaumwa sana.

Sasa, katika lile group, watu karibu wote wanasema wanaamini Mungu. Watu wakaanza yale maneno yao ya imani. Yale maneno ya "tunakuweka katika maombi" "Mungu atakulinda" na maneno kama hayo.

Huko yule mwenzetu anaumwa sana, anatokwa na damu.

Basi mimi nisiyeamini katika uwepo wa Mungu, nikasema Mungu hawezi kusaidia hapa, kwa sababu hayupo.

Nikasema ni wajibu wetu kusaidiana wenyewe sisi watu.

Nikatuma muamala kwa dada mmoja yeye alikuwa ana muda wa kuzunguka chapchap. Akachukua gari, akaenda kwa yule rafiki yetu. Akampeleka hospitali, tena kulikuwa na rafiki yetu humo humo kwenye group daktari hospitali kubwa tu.

Kufika hospitali, yule rafiki yetu daktari akamsaidia mgonjwa, zile hela nilizotuma zikawapa motisha na wale wengine wa "tutakuombea dua" na "Mungu atakuponya" wafuatishe kuchangia, yule rafiki yetu akakatiwa bima ya afya.

Yule rafiki yetu daktari alisema huyu mtu tungechelewa kidogo tu angetuacha, angeaga dunia.

Yani hapo unaweza kuona kabisa imani ya Mungu inavyoweza kuhatarisha maisha ya mtu. Kuna kazi inatakiwa kufanywa na watu, watu wanamuachia kazi Mungu.

Mimi nilikataa ujinga huo wa kumuomba Mungu nikasema hii ni kazi yetu, tuache kumtegea Mungu ambaye hayupo.

Mungu angekuwepo hata magonjwa yasingekuwepo.

Kwa hiyo, ogopa sana mtu anayeamini Mungu.

Anaweza kukuona unakufa kwa kuhitaji msaada, akamuachia Mungu kazi ya kukusaidia. Akasema tu "nakuombea kwa Mungu" na "Mungu atakusaidia".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…