Wabongo tuache unafiki

Wabongo tuache unafiki

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Bila kupepesa macho wala kutikisa kichwa Wabongo tumejariwa unafiki tena wa Hali ya juu.

Hii ni juu ya tukio lililo tokea leo maeneo ya Upanga huko Dar es Salaam.

Ukiangalia comment za wadau juu ya tukio hilo wanaliingiza kwenye mambo mawili tofauti.

Mosi ikiwa ni siasa na pili ikiwa ni uzembe wa Polisi kitu ambacho sicho.

Imagine police walivyo jitahidi kadiri ya uwezo wao wewe mtu ambae upo mbali na tukio unakuja kuanza kuwashutumu polisi eti ni wazembe mara wangemoiga miguuni au mikononi ili wapate kumhoji, hivi mpaka mtu ajitoe hivyo na wewe upige miguu au mikono harafu uende kichwa kichwa unajua kuna nani nyuma yake? Je, kama yeye ni chambo utajuaje?

Hapo ndo anakuja mtu ambaye hata mazoezi ya Mgambo yalimushinda anaanza kumlaumu police.

Watanzania tujitafakari ukiwa sehemu ya tukio ni hali tofauti na aliye JF hivyo kama hujui kausha siyo uanze kulaumu tu.

Pia swala la kuhusisha mara ni mwana chama wa chama fulani kwa kutoa piacha akiwa amevalia sare na kuonyesha kadi ya chama na mbaya zaidi kila mtu anatoa kuwa jamaa wa chama hiki mwingine chama kile.

Kwani tukio analifanya binafsi kama mtu au kama mwanachama? Basi wabongo tujitafakari.

Na pia wengine wameanza kutoa yao eti jamaa alikuwa na ugonjwa wa akili angekuwa timamu asinge fanya hivyo, sawa siwezi wapinga sababu sina uhakika kwa hilo.

Je, siku hizi machizi wanavamia kwa kutumia silaha harafu wanachukua silaha yaani kichaa ametarget hayo yote kweli? Labda ni kweli ila kwa nini tunasema kana kwamba tunaujua ukweli.
Wabongo mjitafakari.

Unakuta hata mwalimu aliye soma kuchambua sentensi kwa njia ya matawi nae analeta porojo hapa eti walikosea, sasa wewe hao ndo wenye taaluma zao waache.

"No research no right to speak kindly be informed" ni hayo tu.

Povu ruksa
 
Duh, kwa jamaa alivyokua slow sana lazima tuwalaumu, jamaa wala hakua na mishe nyingi pale ktk eneo la tukio, walikua wanao uwezo mkubwa tu wakumkabili kabla ya madhara, ingelikua ni wapinzani ungeliskia washapotezwa kitambo coz askari wanaogopa katiba mpya
 
Duh, kwa jamaa alivyokua slow sana lazima tuwalaumu, jamaa wala hakua na mishe nyingi pale ktk eneo la tukio, walikua wanao uwezo mkubwa tu wakumkabili kabla ya madhara, ingelikua ni wapinzani ungeliskia washapotezwa kitambo coz askari wanaogopa katiba mpya
Dah wewe wasema waulize wenyewe utajua kwa nini.
 
Sio wabongo tuache unafiki, CCM ndio waache unafiki na uongo. Jamaa alikua mwana CCM kindakindaki, ila baada ya tukio wamemtengenezea kadi ya Chadema kwa kuedit picha na jina ili kuonesha dunia upinzani ndio wahalifu.
IMG-20210825-WA0024.jpg
 
hv kweli unatetea polisi kwenye hilo tukio,mtu mmoja mapolisi zaid ya 30 na kafunga mtaa kwa masaa.Je wangekuwa watano si mji mzima ungesimama sku yte ya leo
Mkuu je unajua chanzo cha Tatizo?
Je, ulikuwepo kwenye tukio? Kwa nini tunapenda kuwalaumu kisa hatuwapendi.
 
Sio wabongo tuache unafiki, CCM ndio waache unafiki na uongo. Jamaa alikua mwana CCM kindakindaki, ila baada ya tukio wamemtengenezea kadi ya Chadema kwa kuedit picha na jina ili kuonesha dunia upinzani ndio wahalifu.View attachment 1908441
Mkuu hata picha hapo juu ni edit.
Kana unafahamu mambo ya edit utajua tu, jaribu kuangalia kichwa na shingo utapata dots
 
Kwenye hili suala mwalimu aliyesoma kuchambua sentensi kwa njia ya matawi na aliyesoma Fizikia wana tofauti gani? Au unamaanisha nini?
Screenshot_20210825-161557.jpg
 
Back
Top Bottom