Wabongo wampiga Majungu Lulu Diva

Mlokomalia hii ishu ni wanaume
Wakati nyie ndio kwanza mnasahau nyumbani
 
Changanya bajeti za pampers na dawa za maumivu zikiwa fixed kila siku for 5 years. Chukua 20,000×30×12×5= 36,000,000. Hapo inaweza kuwa dawa, pampers, na sabuni za usafi kwa ajili ya mama bila kuhusisha matumizi mengine.

Watu wasifanye masihara

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Kuna baadhi ya watu maarufu awana hela kwakweli japo ni maarufu.
Ukimuondoa Afande Sele mfalme wa rhymes waliowengi wanatumia zaidi ya robo tatu ya kipato chao kidogo kuishi maisha ya kuigiza ilhali mama na baba wanamamaisha magumu.
 
Wengine tangu tuzaliwe hatujawahi timba vijijini kwetu

Kwetu ni hapo dar tutazeekea na kuzikwa dar
 
Point ni moja tu AACHE KU FAKE MAISHA....
Sasa km huko Muheza Ni kwa wajomba na pengine mamake hakuwa na shamba Wala kiwanja ataenda huko akajenge kwa nani.Halafu kazaliwa peke yake, angeenda kujenga huko kwa ajili ya nani na mama anaishi naye Dar.Na yule ni mtoto wa kike usisahau hilo.

Yy ana makazi Dar na alimchukua mama yake kuishi naye na zaidi kumuuguza hadi kufariki. So kwake ni DSM. Kwa wajomba kunamhusu nini kwenda kujenga huko.

Pamoja na hayo, huyo Lulu ana maisha gani makubwa ya kumlaumu kiasi hicho. Au tu kwasababu ja jina kubwa na mavazi basi imekuwa nongwa.

Nafuu hata yeye ana pakujihifadhi hapo mjini. Wangapi majina makubwa na hawana hata kiwanja cha hatu 2,wanamiliki pea kadhaa za viatu na magauni bila kusahau mahawara.

Mwacheni dada wa watu.

By the way yote hii Ni umaarufu unamponza. Unadharauliwa na mtu ambae hajui choo cha shimo kinajengwaje.
 

Kama kuna mtu hatoelewa haya uliyoyaandika,basi tena,tutakuwa kama tunapaka rangi upepo kuwaelewesha.
 

Aisee,huyu Binti kwangu mimi ni mfano wa kuigwa kwa vijana wa umri wake.Wengi sana hawawezi hata kuhudumia kwa mwezi mmoja,achilia mbali muda wote huo aliouguza.Nina Imani Mwenyezi Mungu atamfungulia zaidi milango ya riziki ili aweze kuyatimiza yale yote aliyoshindwa kuyatimiza kipindi anauguza Mama yake.
 
Mwacheni dada wa watu.

By the way yote hii Ni umaarufu unamponza. Unadharauliwa na mtu ambae hajui choo cha shimo kinajengwaje.

Na huu ndiyo ukweli wenyewe.Wanamdharau wakati hata pa kuishi hawana,wako kwa washkaji au kwa Mjomba na Shangazi wamehifadhiwa.
 
Halafu hawaelewi Africa sio kila kijiji unaweza jenga kiurahisi. Kuna maeneo Ukiingia anga zao vibaya unaondoka wewe unaacha mgonjwa anajiuguza. Kuna viijiji ni wachawi hawataki hata nyumba ya bati ijengwe. Haya yote tumeyaona. Halafu ndio itokee kijana mdogo unaenda kufanya matusi mbele ya wazee.

Na tabia ya wadigo hawajali walikosana ama hawakumuuguza ndugu yao akifa wanataka wamzike wao no choice. Hata kwa Lulu lazima wajomba walimtaka ampleke mama yake kule. Na hii ipo vijiji vingi ili kumkomoa mtu

By the way sio lazima kujenga kijijini iliko asili yako. Unaweza mjengea mzazi mjini na mkaweka utaratibu wa kuzikwa hapo kwenye mji mpya ya kijijini mkayaacha huko.

Lakini Ugonjwa mzito wa kudumu ama vifo havipigi hodi wakati na siku yoyote vinalipuka na unakosa la kufanya zaidi ya kushika lililokufika

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 

Ile tu kuamua kumchukua Mama yake Mzazi na kuja kuishi nae hadi umauti unamkuta ni Sadaka tosha kabisa kwake kuliko hata kujenga huko Kijijini,wanaolaumu ningewaelewa kidogo kama Mama yake angekuwa anaugulia huko Kijijini hadi umauti unamkuta huku yeye Lulu akiwa mjini anakula Bata.Lakini Binti kaamua kuteseka na Mama yake hadi hatua ya mwisho,halafu bado watu wanabeza, inasikitisha sana.
 
Amemaliza kazi yake ajiangalie yeye na furaha yake kwa sasa

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Wabongo hapana kwa kweli lol, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
L
Point nyepesi sana hii wala haireflect uhalisia tunaouongelea hapa,nakuuliza ni wapi huyu Binti kafake maisha,kama angefake wewe ungeweza kuona hata hiyo nyumba ya Bibi yake?

Umaarufu umemponza...
 
L



Umaarufu umemponza...

Utakuwa na stress zako wewe na huyu Binti,si bure.Umaarufu umponze vipi,kwa haya maneno ya mitandaoni? Baada ya kumsema amepungukiwa na nini? Amekosa deals za hustles zake anazofanya kila siku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…