Wabongo watengeneza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be From BetaTQ" wenye kufanana na Instagram

Wabongo watengeneza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be From BetaTQ" wenye kufanana na Instagram

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Siku za hivi karibuni mastaa na watu maarufu Nchini Tanzania wameonekana wakitangaza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be from BetaTQ", akiwemo mtangazaji wa burudani za michezo, Shafii Dauda na Mwanasiasa, Mwanaharakati na mtayarishaji wa vitabu Yericko Nyerere wameonekana wakishawishi wafuasi wao kujiunga na mtandao huu mpya.

Chanzo cha Inside Tanzania kimesema mfumo wa kijamii Kuwa kutoka BetaTQ umetengenezwa na kampuni BetaTQ. Ni jukwaa la kijamii lililoundwa kwa ajili ya watumiaji kushiriki maudhui na kushirikiana na wengine katika mazingira ya kidijitali. Programu hutoa vipengele kama vile Kushiriki Hadithi, Machapisho (Video, Picha, Sauti), na kipengele cha Gumzo1.

Kuhusu umiliki, BetaTQ Ltd ni kampuni inayofanya kazi iliyoanzishwa tarehe 3 Aprili 2024, na imekuwa ikifanya kazi tangu kwa mujibu wa takwimu za utafutaji mitandaoni. Kampuni hiyo iko Leicester, Leicestershire, na ina wakurugenzi 2 wanaofanya kazi, ambao ni Mr Hartman Osmund kutoka Uingereza na Mr Neithan Hamis Swed kutoka Tanzania. Hata hivyo, mtu mahususi anayemiliki "Be from BetaTQ" au kampuni mama ya BetaTQ Ltd hakutambuliwa katika matokeo ya utafutaji mitandaoni.

Features za mtandao huu zinataka kufanana na za mtandao wa Instagram karibia kila kitu, unaonekana ni mtandao wa mahudhui ya picha na video tofauti na mtandao kama JamiiForum.

Kinachofanya niamini mtandao huu ni wa Kitanzania ni kutokana na screenshots zilizowekwa pale Playstore kwa asilimia kubwa zinaonesha username au watumiaji wake ni wenye majina ya kibongo. Pia wabongo ndio wanautangaza. Kwa asilimia kubwa huu ni mtandao wa kibongo.

Mtandao huu unaoshesha awali ulisajiriwa Tanzania, lakini ukaondoa huduma zake, kwasasa umesajiliwa China, na Uiingereza na unapatikana mataifa zaidi ya 180 duniani.

Mtandao wa Be umekuja kama mshindani wa Instagram, Tiktok na Facebook, lakini una vitu vingi vya ziada ambayo huwezi kuvipata kwenye mitandao mingine. Mfano unaweza kuandika post kwa njia ya sauti, na ukajibu reply kwa njia ya sauti vilevile, Hii huwezi kuipata huko Instagram au Facebook, Pili kwenye huu mtandao unaweza kuandaka makala kwakuweka cover kama kitabu hivi na unaweza kuuza makala zako kupitia mtandao huu huu, yaani kuko kama amazon vile.
Mtandao una mahadhi ya kitz ama una ladha ya kiafrika flani hivi.

Nimejiunga katika mtandao huu, na nimeona mataifa mengi yamejiunga katika mtandao huu watu wanapost biashara zao kama instagram au fb, watu wanapiga soga kwa sauti badala ya kuandika muda wote, Ni mtandao mzuri sana.

For the national security Wizara ya Mawasiliano chini ya @napennauye ishawishi wamiliki wa mtandao huu waufanye kuwa wa kitanzania zaidi utasaidia kiusalama huko mbeleni, I know mitandao ya kijamii yote duniani hukusanya taarifa za watu, sasa kama mtandao huu uliwahi kuwepo Tz na umeamua kwenda Uingereza na China basi ni uzembe wetu kulinda vitu zivizuri kama hivi ambayo vitakuja kuwa muhimu kwa taifa kesho!

Mtandao huu ukifanywa kuwa na makao hapa Tanzania maana yake taifa litakuwa limejihakikishia usalama zaidi wa information tofauti na leo Instagram, fb, Tiktok, Whatsapp nk ambapo wanakusanya taarifa za Watz na hakuna ajuae wanazipeleka wapi na wanazitumiaje huko.

Screenshot_20240413-063509.jpg

Screenshot_20240413-063515.jpg

Screenshot_20240413-063522.jpg

Screenshot_20240413-063527.jpg
 
Siku za hivi karibuni mastaa na watu maarufu Nchini Tanzania wameonekana wakitangaza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be from BetaTQ", akiwemo mtangazaji wa burudani za michezo, Shafii Dauda na Mwanasiasa, Mwanaharakati na mtayarishaji wa vitabu Yericko Nyerere wameonekana wakishawishi wafuasi wao kujiunga na mtandao huu mpya.

Features za mtandao huu zinataka kufanana na za mtandao wa Instagram karibia kila kitu, unaonekana ni mtandao wa mahudhui ya picha na video tofauti na mtandao kama JamiiForum.

Kinachofanya niamini mtandao huu ni wa Kitanzania ni kutokana na screenshots zilizowekwa pale Playstore kwa asilimia kubwa zinaonesha username au watumiaji wake ni wenye majina ya kibongo. Pia wabongo ndio wanautangaza. Kwa asilimia kubwa huu ni mtandao wa kibongo.

View attachment 2961973
View attachment 2961974
View attachment 2961975
View attachment 2961976
Hapo wabongo developers ndipo huwa wananiacha hoii. Kwa features kama za instagram ni vigumu kumshawishi mtu kuacha instagram aje kwenye huo mtandao na adumu. Watakachobaki kusena ni tuwe wazalendo tutumie vya kwetu. Hatutumii products kisa nibza kwetu bali tunatumia products kwa sababu ni nzuri.
Watu hatutumii jf kisa ni ya kitanzania bali ni kwa sababu ni unique na tunapata kitu tofauti
 
Tuwasapoti tu, uwezi kujua labda badae utafanya vizuri zaidi na kuwa kama Tiktok... Cha msingi tusapotiane kama wabongo tufike kule Marekani ilikofika, tuwe nchi ya mfano barani Afrika
Narudia tena. Watu hawatumii products kisa kukusupport ukitegemea hilo mtu ataitumia mwezi baadaye inabaki tu kwenye simu bila hata kufunguliwa. Yalitokea kqa pamoja app, mayoco na apps kibao. Watu wanatumia products kwa sababu wameipenda ina kitu unique.
Jiulize kwanini watu siku hizi wanapenda suti za kushona hapa hapa kuliko za kununua from uturuki?
Ni kwa sababu siku hizi suti za kushona ni nzuri.
So tengeneza kitu kizuri sio una clone tu vitu ukitegemea support utafail unless serikali izipge pin hizi app za nje tulazimike kutumia made in tz.
 
Keyword ni Kijamii....

Sasa kama Huko Insta kuna Jamii kubwa zaidi na hata jamii ya huku na kule inapatikana unategemea nini ? Pili kama hauna monetization nzuri au back-up ya investors unaweza kujikuta unachoma pesa bila kupata return on investment...
 
Wabongo tunafeli vitu vidogo sana hata kuangalizia hatuwezi, JINA GANI REFU NA GUMU HIVYO??

Marketing na Ubinifu ni zero kabisa, Jina refu kama Mzizi wa bangi

Nataman nikawachape vibao, Shenzi kabisa...
Mtandao unaitwa "BE", kule playstore wanaandika Be from BetaTQ hili iwe rahisi kupatikana au kuona App kwa sababu uki-search "BE" pekee zinakuja App tofauti, ndio naana wakaweka jina refu hili ukisearch ije haraka ila ukipakua jina linabaki "Be"
 
Ok
 
Back
Top Bottom