Wabongo watengeneza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be From BetaTQ" wenye kufanana na Instagram

Wabongo watengeneza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be From BetaTQ" wenye kufanana na Instagram

Kinachofanya niamini mtandao huu ni wa Kitanzania ni kutokana na screenshots zilizowekwa pale Playstore kwa asilimia kubwa zinaonesha username au watumiaji wake ni wenye majina ya kibongo. Pia wabongo ndio wanautangaza. Kwa asilimia kubwa huu ni mtandao wa kibongo.
Una usalama kiasi gani kwa mlaji!
Wamiliki ni watu wa mlengo gani?
Tuanzie hapo
 
Mi sitaki huo ujinga sio unaenda kujiunga huko mara unakuta mwashambwa ni content controller mara cjui ni platinum member,,, yaani mi niende huko nikawe mnyonge no thank you!!!
 
Tatizo linaanza ukishafanikiwa wao ndio wataanza kutuvimbia sisi na kujiona wao ndio wajanja, wabongo tuna mambo ya ovyo sana
Nimeipata comment niliyokuwa naitafuta 😂😂😂
Wabongo tuna roho za korosho sana ndio hasili yetu hii wote tuwe chini no kuvimbiana
 
Tatizo linaanza ukishafanikiwa wao ndio wataanza kutuvimbia sisi na kujiona wao ndio wajanja, wabongo tuna mambo ya ovyo sana
Attitude ya mtu mweusi ndio kama hii ya kwako which is roho mbaya
 
Siku za hivi karibuni mastaa na watu maarufu Nchini Tanzania wameonekana wakitangaza mtandao mpya wa kijamii unaoitwa "Be from BetaTQ", akiwemo mtangazaji wa burudani za michezo, Shafii Dauda na Mwanasiasa, Mwanaharakati na mtayarishaji wa vitabu Yericko Nyerere wameonekana wakishawishi wafuasi wao kujiunga na mtandao huu mpya.

Chanzo cha Inside Tanzania kimesema mfumo wa kijamii Kuwa kutoka BetaTQ umetengenezwa na kampuni BetaTQ. Ni jukwaa la kijamii lililoundwa kwa ajili ya watumiaji kushiriki maudhui na kushirikiana na wengine katika mazingira ya kidijitali. Programu hutoa vipengele kama vile Kushiriki Hadithi, Machapisho (Video, Picha, Sauti), na kipengele cha Gumzo1.

Kuhusu umiliki, BetaTQ Ltd ni kampuni inayofanya kazi iliyoanzishwa tarehe 3 Aprili 2024, na imekuwa ikifanya kazi tangu kwa mujibu wa takwimu za utafutaji mitandaoni. Kampuni hiyo iko Leicester, Leicestershire, na ina wakurugenzi 2 wanaofanya kazi, ambao ni Mr Hartman Osmund kutoka Uingereza na Mr Neithan Hamis Swed kutoka Tanzania. Hata hivyo, mtu mahususi anayemiliki "Be from BetaTQ" au kampuni mama ya BetaTQ Ltd hakutambuliwa katika matokeo ya utafutaji mitandaoni.

Features za mtandao huu zinataka kufanana na za mtandao wa Instagram karibia kila kitu, unaonekana ni mtandao wa mahudhui ya picha na video tofauti na mtandao kama JamiiForum.

Kinachofanya niamini mtandao huu ni wa Kitanzania ni kutokana na screenshots zilizowekwa pale Playstore kwa asilimia kubwa zinaonesha username au watumiaji wake ni wenye majina ya kibongo. Pia wabongo ndio wanautangaza. Kwa asilimia kubwa huu ni mtandao wa kibongo.

Mtandao huu unaoshesha awali ulisajiriwa Tanzania, lakini ukaondoa huduma zake, kwasasa umesajiliwa China, na Uiingereza na unapatikana mataifa zaidi ya 180 duniani.

Mtandao wa Be umekuja kama mshindani wa Instagram, Tiktok na Facebook, lakini una vitu vingi vya ziada ambayo huwezi kuvipata kwenye mitandao mingine. Mfano unaweza kuandika post kwa njia ya sauti, na ukajibu reply kwa njia ya sauti vilevile, Hii huwezi kuipata huko Instagram au Facebook, Pili kwenye huu mtandao unaweza kuandaka makala kwakuweka cover kama kitabu hivi na unaweza kuuza makala zako kupitia mtandao huu huu, yaani kuko kama amazon vile.
Mtandao una mahadhi ya kitz ama una ladha ya kiafrika flani hivi.

Nimejiunga katika mtandao huu, na nimeona mataifa mengi yamejiunga katika mtandao huu watu wanapost biashara zao kama instagram au fb, watu wanapiga soga kwa sauti badala ya kuandika muda wote, Ni mtandao mzuri sana.

For the national security Wizara ya Mawasiliano chini ya @napennauye ishawishi wamiliki wa mtandao huu waufanye kuwa wa kitanzania zaidi utasaidia kiusalama huko mbeleni, I know mitandao ya kijamii yote duniani hukusanya taarifa za watu, sasa kama mtandao huu uliwahi kuwepo Tz na umeamua kwenda Uingereza na China basi ni uzembe wetu kulinda vitu zivizuri kama hivi ambayo vitakuja kuwa muhimu kwa taifa kesho!

Mtandao huu ukifanywa kuwa na makao hapa Tanzania maana yake taifa litakuwa limejihakikishia usalama zaidi wa information tofauti na leo Instagram, fb, Tiktok, Whatsapp nk ambapo wanakusanya taarifa za Watz na hakuna ajuae wanazipeleka wapi na wanazitumiaje huko.

View attachment 2961973
View attachment 2961974
View attachment 2961975
View attachment 2961976
Achana na hivyo vitu vya kibongo vitakuja kukuponza. Je, ina usalama kwa watumiaji kama ilivyo instagram? Take care!
 
Shida ni kwenye usalama wa data zetu tu maana hii bongo kwa sasa watu wanawafanyia kazi ma godfather wao
 
Back
Top Bottom