Waboreshaj saidia: kuuza mboga za majan packed!

Waboreshaj saidia: kuuza mboga za majan packed!

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Tunakubaliana kuwa watu weng baada ya corona wamejua thaman ya kula kwa afya ikiambatana na kula zaid vyakula vya asili vyenye virutubisho muhim na kwa wingi.
Sasa mimi nina ndoto ya kufunga mkusanyiko wa mboga za majan na mitishamba -dawa, kwa kuzicompress zikawa katika mfumo sausage kubwa. Yani ujilie mboga za majan bila kusubir kwenye mlo! Na hasa zikiwa mbichi kias.
Mwenye mawazo ya kitaalam kuhusu packaging na utunzaj anishaur. Nataman niwe na kiwanda kinachohitaj mboga za majan kwa wing nje na ndan ya dar.

....Faida za mboga za majan (nimecopy kwa member verykeys)
1. Vitamini kwa wingi
2 . Madini kwa wingi
3. Dawa zinazotokana na mimea kwa kulinda afya.
4. Mboga za majani zinasaidia kukinga mwili kwa magonjwa mbalimbali
5. Mboga za majani pia husadia kupunguza, kurekebisha na kuweka uzito sawa.

Tuangalie sababu kubwa zinazofanya mboga za majani kupunguza uzito wa mwili ili kuwa na afya bora:

1. Mboga za majani zina mafuta kidogo sana. Mafuta yake yayenyushwa vizuri na joto la mwili kuliko mafuta yatokanayo na mboga za vitoweo vya nyama.

2. Mboga za majani zina nguvu ukaa kidogo sana kulinganisha na mboga zingine kama nyama. Nguvu ukaa zikiwa nyingi mwilini kutokana na chakula zinakuwa mafuta mwilini ambayo unanepa sana na uzito kuongezeka mwilini.

3. Zinaongeza maji kidogo kidogo mwilini kwa sababu mboga za majani zina madini ya sodium kwa wingi.

4. Mboga za majani zinashibisha haraka na kujaza tumbo mapema kwa sababu ya umbirorojo au cellulose

5. Zinaongeza uhai au “vitality” kwa sababu zina virutubisho vingi muhimu kwa mwili.

Kwa hiyo mboga za majani zina sifa zote za kukufanya upunguze uzito kwani zina vitamini nyingi sana na madini ambayo ni muhimu katika kuufanya mwili wako uwe na afya nyama muda wote.

Pia mboga hii zina kemikali rafiki kwa mwili kwa kuponyesha magonjwa na kuufanya uwe na kinga nzuri sana dhidi ya magonjwa mengi.

Mboga hizi pia hunyonya mafuta toka utumbo mwembamba kwa sababu ya nyunyuzi au umbijani rojorojo au cellulose ambayo zina nyunyuzi kwa wingi. Pia mboga hizi zina mafuta kidogo sana ambayo joto la mwili nyuzi 36.7 centigrade linayeyusha mafuta hiyo kwa urahisi sana.

Mboga hizi pia zina tu nguvu ukaa kidogo sana ukilinganisha na vyakula vingine. Mafuta yatokanayo na mboga huwa hayagandi katika damu ndani ya mishipa ya damu tofauti na mafuta yatokanayo na mboga za nyama ambayo huganda na kuzuia damu ndani ya mishipa yetu ambayo husababisha vifo vya kushtukiza.

Mafuta ya mboga yanayeyushwa na kuuguzwa kwa hiyo hayakai mwilini katika mfumo wa mafuta “fat”. Mwili unakuwa si wa kunenepa bali unakuwa na afya nzuri yaani mwembamba na mrembo zaidi.

Mboga mboga za majani zina madini muhimu ya sodium kupunguza maji mwilini. Mwili ukiwa na maji mengi unakuwa mnene na mzito kuliko kawaida yake. Kwa hiyo mboga mboga za majani ni muhimu kwa kupunguza maji mwilini na kupunguza uzito.

Mboga mboga hizi zinashibisha mapema na kujaza tumbo ambapo inafanya upate choo vizuri zaidi. Inazuia kuvimbiwa kuliko vyakula vingine. Mwisho zinaongeza uhai kwa sababu ya sifa zake. Watu wanaoishi muda mrefu ni wenye kula mboga mboga kwa wingi.
 
Back
Top Bottom