Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WABUNGE 35 KWENYE MAFUNZO YA APSEZ NCHINI INDIA
Wabunge 35 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kamati mbalimbali za Bunge hilo wapo katika ziara ya mafunzo Nchini India, kujifunza kuhusu ushirikishaji wa Sekta binafsi katika Uwekezaji, Usimamizi na Uendelezaji kwenye shughuli za bandari kutoka APSEZ, ambayo ni kampuni kubwa iliyowekeza Katika Bandari 13 ndani na nje ya India.
Wabunge hao wameongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, ambaye katika mafunzo hayo ametoa maelezo ya utangulizi kuhusu ziara ya Mafunzo kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliotembelea Makao Makuu ya kampuni ya Adani Ports and Special Economic Zone Limited ( APSEZ) mjini Ahmedabad, Jimbo la Gujarat Nchini India.
Baadhi ya Wabunge hao walioshiriki mafunzo ya APSEZ Mjini Ahmedabad ni pamoja na Mhe. Prof Makame Mbarawa (Waziri), Mhe. Atupele Mwakibete (NW), Mhe. Juliana Shonza, Mhe. Rose Tweve, Mhe. Nicholaus Ngassa, Mhe. Lucy John Sabu, Mhe. Erick Shigongo, Mhe. Festo Sanga, Mhe. Kasalali Mageni, Asia Halamga na wengine wengi.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-03-11 at 13.37.45(1).jpeg39.6 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-03-11 at 13.37.45(2).jpeg47.9 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-03-11 at 13.37.47(1).jpeg45.8 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-03-11 at 13.37.48.jpeg33.2 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2023-03-11 at 13.37.45.jpeg31.4 KB · Views: 5