Kichuguu,
Mkuu nakubaliana sana na maelezo yako na hakika hii habari nzima inaonyesha wazi jinsi JK alivyokuwa na wakati mgumu ndani ya chama chake..
Kinachonishinda mimi kuelewa ni hizi kampeni kupingwa na wana mazingira kama kweli zipo..
Naweza kukubali kuwepo kwake kwa sababu zilizotolewa kwani chombo hiki cha Haki za binadamu na mazingira kipo mikoa yote na huyu mchungaji ni msemaji mwakilishi wa chombo hicho hivyo sii mawazo yake binafsi ila yeye ni mwakilishi wa mawazo ya wanaharakati wa chombo hicho..
Hadi hapa, sioni kosa lolote la huyu mchungaji ikiwa anaifanya kazi yake..
Tatizo linakuja naposoma habari nzima kuhusu hawa mawaziri 13 na Wabunge 46 ambao wameshindwa kuwakilisha mawazo yao bungeni badala yake wanaendesha kampeni chini chini huko mikoani..
Kimsingi madai yao yana nguvu sana hasa wanaposema kuwa Rais ajiuzulu kwa sababu Serikali yake imeshindwa kutekeleza maazimio ya Bunge..
Hii sababu kama ingeandamana na maelezo kamili yanayohusiana na maazimio ambayo yalipitishwa na bunge JK kashindwa kuyatekeleza ingetusaidia sana wananchi kuelewa zaidi kwani hadi leo hii madai mengi ya wananchi yanatokana na ahadi za JK, sio maazimio yaliyopitishwa na bunge letu...
Sasa ikiwa hawa wabunge na mawaziri ni katika fungu la Mafisadi ningependa sana kuelewa hayo maazimio yaliyopitishwa ambayo JK kashindwa kuyatekeleza..Ina niuwia vigumu kufikiria kwa fikra zangu hawa Mafisadi wanaweza vipi kuendesha kampeni kama hizi wakati JK anafanya kila analoweza kuwalinda. Je, ni Maazimio yapi hayo!
Na sio kweli kabisa kuwa JK ni kiongozi bora kuliko wote ama amekuwa na wakati mgumu kuliko Nyerere.. Haya ni matusi kwa mwalimu, JK amepewa nchi ikiwa katika hali nzuri sana kiuchumi na kama tunazungumzia Mafisadi tukumbuke tu kwamba Ufisadi ni kama crimes nyingine zozote zile. Zilikuwepo na zitaendelea kuwepo isipokuwa kusimamisha kwa sheria ndio njia pekee ya kulinda na kuondoa maradhi haya..
Lowassa, Rostam kina Patel na wengine wote ni kizazi kipya cha Ufisadi ambao wameibuka baada ya sisi kuachia milango wazi hata iwe kwa amri ya Mkapa..Nina hakika kama JK au Mwinyi au Mkapa ndio wangeutafuta Uhuru wa Tanzania basi hadi leo hii tungekuwa tukitawaliwa na hawa wote wasingeweza Upinzani wa kina Fundikira, Marealle, Mtenvu na mgawanyiko wa makabila yote tulokuwa nayo.. nasema hivi jamani, temea mate chini, umlaani shetani kwanihawa wote kina Mwinyi, Mkapa na JK wameikuta nchi imeshawekwa sawa...
JK anaweza kabisa kupunguza au hata kusimamisha Grand Corruption kwa siku moja kwa sababu wahalifu wanafahamika na ushahidi upo wazi kabisa... hakuna mtu anayemlaumu JK kwa kushindwa kuondoa corruption, haya niu maradhi hayawezi kwisha kabisa kwani crimes ni sawa maradhi ya binadamu, mfano wa Maleria..Hatuwezi kabisa kuondoa mardhi haya ikiwa mbu wataendelea kuzaana na hakuna jitihada zinazofanywa kuzuia mbu kuzaana, kinga na hata dawa za mbu..Mfumo wa utawala wa JK hivi sasa umeshindwa kabisa kufanya hata mojawapo ktk kupambana na Ufisadi zaidi ya kutambua tatizo la kuwepo maradhi haya..
Sifa zote anazopewa JK ni kutokana na kutambua kwake au niseme kukubali kuwa Tanzania ina tatizo kubwa la corruption lakini ameshindwa kabisa kuzuia mafisadi kuzaana. kuweka kinga na hata kutumia dawa ya kuua mafisadi ambayo ni kuwafikisha mahakamani akiendelea kudai kufanya utafiti zaidi...hali tayari serikali yake imesha toa diagnosis kuwa maradhi haya yapo na ndiyo yanayoua uchumi wa nchi yetu..
Jamani, tujiulize sote pamoja na mapenzi yetu kwa rais, chama au hata nchi yetu.. Kikwete ameweza kufanya nini ktk vita dhidi ya Mafisadi ili kukinga, kuzuia au hata kupambana na ufisadi ikiwa vyombo vilivyopo havitendi kazi yake kabisa!..
Tunachokiona kila siku katika magazeti ni vita baina ya mafisadi na wazalendo, Hivi kweli Kikwete akiambiwa Kipindupindu kimeingia Mbeya na kimeisha ua watu bado atataka ushahidi upi ikiwa wanamazingira watamwambia virusi vya Kipindsupindu vimebainika, bado atahitaji ushahidi gani zaidi..au kwa sababu hapa ana deal na maswahiba wake!.. imekuwa kama hadithi ya Wakerewe hawawezi kumuua nyoka Chatu, hata kama huyo nyoka amemeza mbuzi wake kwa sababu wanaamini kuua Chatu ni mkosi ktk familia..
Hivyo ni kweli JK anachemsha lakini naposikia kwamba hawa mawaziri na wabunge ni ktk kundi la Mafisadi nashindwa kuunganisha kabisa kwani JK amewalinda sana na hakika mdanganyika kwa hulka hana shukran..
Mtu kama Lowasssa aemjaa chuki miaka yote, hana rafiki isipokuwa kwa yule anayemwabudu yeye. Ukiwa mshindani wake tu iwe hata kimawazo basi wewe ni adui yake na yupo tayari kutumia kila njia ktk uwezo wake akumalize!..
Pamoja na yote haya ningependa sana kuelewa hawa wabunge na mawaziri wanapotaka JK ajiuzulu wao wanataka nani ashike nchi badala yake.. Shein au Sitta!..

Last edited: