Wabunge 46 na mawaziri 13 wahamasisha wananchi kutaka JK ajiuzulu

 
Waswahili husema ukiona moshi wafukuta, ujuwe moto waja...

Mkuu heshima mbele

Sio lazima moto uje na isitoshe waliouanzisha wamekosea step na sasa hivi hata wafanyaje hawezi kupata Iman kutoka kwa wananchi ni bora tuuu wakae pembeni kubakia kuwa watazamaji maana wasije wakaishia lupango.

Unajua wabunge wengi ni wanafiki na isitoshe kila mmoja wao hasa wa chama tawala wanafikiria ni jinsi gani watapata vyanzo vya fedha kwaajili ya uchaguzi ujao ndio maana wanatapa tapa (Empty heads) sasa tegemeo hasa ni kwa wahusika wakuu. Ila mwenzao yupo One Step Ahead.

Acha tuangalie alama za nyakati

Mkuu Rev Respect
 

Mkuu wangu unaniuliza maswali ambayo majibu yake unayo mwenyewe. Bunge letu ni BURE hilo wazi na hata Dr.Slaa kisha sema mara kibao kuhusiana na sheria za kumwondolea kinga Mkapa. anajua fika kura zinazotakiwa haziwezi kupatikana..na pengine hata hiyo hoja kutokubaliwa kuzungumzwa. Na kikubwa tukumbuke kwamba wapinzani wa Lowassa bungeni sii wapinzani wa Mkapa hii ikiwa ni pamoja na JK mwenyewe..Binafsi naamini kabisa kwamba Sitta ni mpinzani wa Lowassa lakini sii wa Mkapa, na bila shaka anapenda sana kumweka kitimoto lakini wakiweza kumsimamisha Lowassa madhambi ya kina Mkapa na wengineo wote tayafikishwa bungeni.

Kwa hiyo sii swala la udhaifu wa JK ktk maswala ya Ufisadi ila tatizo hili lina mizizi ndani ya chama..Soma maelezo ya ndugu yetu ChiefMtz hapojuu utaelewa kwamba mzizi wa Ufisadi nchini haukuanza jana. Na nimewahi kusema kwamba yotew yaliyotokea sii kwamba yalitokea kwa bahati mbaya..hapana mkuu, Yalipangwa na mikakati ikapangwa kuhakikisha wazee hawa hawatakufa maskini..

Takukuru hawawezi kufanya kitu chochote kwani hawana nguvu hizo. Sii chombo huru ila wanaambiwa cha kufanya kinyume cha taratibu na sheria unazofikiria wewe na mimi..Hivyo kama kweli tunataka sheria isimame hatuna haja wala sababu ya kumsubiri JK, RO au mtu mwingine yoyote kwani hakuna mtu ndani ya CCM mwenye ubavu wa kusimamisha Ufisadi.. nasema HAKUNA mtu hata mmoja na itakuwa ujinga kupiga kelele kuhusu JK wakati tukijua fika kwamba hakuna mtu badala yake..Ni sawa na kuondoa tairi lenye pancha wakati huna spare tire linalo fit!.
Kwa hiyo kumsema JK wakati chama hakina mtu mwenye uwezo wala moyo wa kukiuka maagizo ya wazee wa CC sijui kama kweli tunatumia akili zetu sawasawa...

Kumbuka tu kila mtu atakaye gombea Urais kiti cha CCM ni lazima apitishwe na wazee wetu ambao ni pamoja na Mwinyi na Mkapa.. hakuna chaguo la wananchi ama chaguo la wanachama wa CCM ila rais wetu hutokana na chaguo la kundi dogo sana la watu ndani ya chama CCM... hawa wazee wanaweza kumsimamisha hata Kigunge kugombea kiti cha Urais na tusiweze kubadilisha kitu..Those are the fact, hivyo JK lazima alikubaliana nao mambo fulani ambayo hawezi kupindisha na nina hakika Ufisadi wao ni ktk ahadi hizo ndio maana wote mnaolalamikia Ufisadi mnaitwa - Mijitu mingine ina wivu wa kijinga!
 
Last edited:
Mh, Mkandara

well nimeisoma post yako na nimeilewa vizuri, hila kama nitakua mkweli amna jipya kama ulivyosema mwenyewe hapo kwangu. Nianze na kusema ni wewe ndie uliesema ya kwamba sio lazima bunge tu ata takuruku wanaweza fanya kazi ya kukamata mafisadi nadhani jibu lako la pili ni kazi bure tu hiyo takuruku yenyewe kitu ambacho nimeongelea na bunge ambalo kwa sasa amna mtanzania mwenye akili timamu akajua kwamba wabunge hawana faida na wezi wenyewe wengi ndio wamo jumba hilo hilo.

kitu cha kuzingatia ambacho wengi wetu tunakwepa kuangalia ni kiini cha tatizo lenyewe inavyoonekana wengi tuna amini hawa wazee wetu uliowataja na hata viongozi wengine wa high profile ni kama semi prophets wetu. Hivyo sauti zao au jinsi wanavyotuchagulia viongozi, na mambo yao ya kuendesha nchi kwa namna za shagla-bagala ni sawa tu kisa ni mwinyi au mkapa au Mh, yeyote yule labda ndio maana hata huyo raisi wetu tunamwita mtukufu. tumewafanya hawa watu untouchable kisheria, kwa kuwa wao ni binadamu kama mimi na wewe message tunayowapa ni kwamba hata ukiiba, ukijichukulia mali ya watanzania ukajipa mwenyewe, ukigawa assets zao hovyo ni sawa baadae we uguswi sasa kama sisi kweli ni watu wenye akili timamu na bado tuna ona sawa hii fitna aiwezi hisha milele. na chanzo chenyeweni hizo power zetu tulizowapa hawa watu. Hewala mpaka lini mkuu.

ndio hapo sasa mimi naona ni wakati wa kujirudishia baadhi ya haki zetu, na hilo lianze na kuunda vyombo vingine vya kisheria vyenye uwezo wa kupambana na uhalifu kwanza hiyo si kazi ya bunge katika nchi nyingi duniani bali africa tu na nchi chache. na katika vyombo hivyo amna mtu atakaekuwa above the law. Politics is politics asikudanganye mtu yakuwa amna siasa duniani isiokuwa ya urafiki, amna bunge lisilo kuwa na wanafiki ndani ya chama kisa mtu wao hayupo juu, thats the nature of politics. lakini politics ya kusema marafiki wote tuibe hiyo si politics bali ni wizi wa mali zetu.

na mwisho nimalizie na kusema yes ni kweli tatizo lenyewe sio JK, yeye ni product ya sheria ya na nguvu alizopewa, kama ulivyoona Mwinyi, Mkapa na atakae mfuata JK atakua hivyo hivyo mpaka lini tukubali upuuzi huu. Ni kweli nakubaliana na wewe wezi ni wengi na hali halisi kuwashika wote labda uivunje na serikal yenyewe kitu ambacho ni impossible or a mammoth asking. lakini kitu ambacho tunaweza kuanza nacho ni kugawa nguvu za bunge na za raisi sehemu nyingine na mkono wao usifike huko sio sehemu moja tu tatu hata nne.
 


Kiongozi wa nchi (Rais) haiongozi nchi peke yake huwa anawashauri wa chini na washauri wakuu wa kumshauria. Katika hao Wabunge nao wanahusika moja kwa moja kumshauri Rais sasa mimi nashindwa kuelewa kama wanamshauri na yeye hawasikilizi wanahaki kabisa ya kumshauri ajiuzulu. Kwa upande wangu bado sijaona kama Rais anastahili kujiuzulu namwona ni mtu msikivu na anaeshaurika ila upole amezidisha kwa watendaji wake, inaonekana wanamdanganya sana.
Hao wabunge kama wanataka hivyo wafanye wenyewe uwezo wa kikatiba wanao wasitutumie wananchi kama chambo wananchi hatuna uwezo wa kikatiba wa kumwondoa Rais wa nchi kwa haraka kama wao.
 
nyumba bora ujengwa kwa msingi bora kuanzia mwanzo.maneno yako ni ya kampeni zaidi kuliko ukweli.kuna mambo mengi ya kutatuliwa ambayo hayakuitaji kusubiri awamu ya pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…