Wabunge 55 walioidai Tanganyika mwaka 1993 walikuwa Watanzania au walitoka sayari ya Mars?

Wabunge 55 walioidai Tanganyika mwaka 1993 walikuwa Watanzania au walitoka sayari ya Mars?

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa, "kama ingekuwa inawezekana kuwa na Serikali moja, hilo ningeliunga mkono, lakini Wazanzibari hawatakubali".

Mwalimu Nyerere aliona wazi hoja ya kuwa na Serikali 3 au 1, na alijua wazi kuwa Serikali mbili ni nadharia danganyifu, lakini alikuwa na hofu katika machaguo mawili yaliyokuwa halisia:

Serikali 3, Mwalimu alisema ni hofu yake kuwa Muungano unaweza kuvunjika, na yeye hakuwa tayari hilo litokee. Akasema kuwa unapokuwa na Serikali 2, moja ya nchi kubwa kama Tanganyika, na nyingine ya nchi ndogo, pungufu ya wilaya ya Sengerema, ni vigumu muungano wa namna hiyo kuendelea.

Kwenye serikali moja, ambayo ingeifanya Zanzibar, hata kwa upendeleo, kuwa na mikoa labda 2 au 3, Wazanzibari wasingekubali, na huenda wangeona afadhali kujitoa kwenye muungano, na Mwalimu hakutaka kabisa muungano ufe, hata kama wananchi wote wasingeutaka.

Kwa sasa Mwalimu hayupo, mazingira yamebadilika. Tungeweza kuamua kuwa na serikali 1, wazanzibari wasipokubali, tukazanie kuwa na Federation ya East Africa, na Zanzibar iingie humo kama nchi.
Mawazo yako ni mazuri. Kuhusu EA Federation ni vigumu kwa vile kila nchi kwa sasa inapigania Utaifa wake. Wapo viongozi ambao ni wapenda madaraka sana na hivyo ni vigumu kuachia nafasi zao na kuyakasimu kwenye hiyo Federation. Kwa sasa tuna Community ambayo inasuasua. Kuingia kwenye Federation ni ngumu zaidi.
 
Hivi najua Ulimwengu bado yupo wengine akina nani wako hai? wakati huo nan alikuwa Waziri Mkuu? Warioba,Malecela au Salim?

Waziri Mkuu alikuwa Malecela .... hii issue ndiyo iliyosababisha asiupate Urais.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa, "kama ingekuwa inawezekana kuwa na Serikali moja, hilo ningeliunga mkono, lakini Wazanzibari hawatakubali".

Mwalimu Nyerere aliona wazi hoja ya kuwa na Serikali 3 au 1, na alijua wazi kuwa Serikali mbili ni nadharia danganyifu, lakini alikuwa na hofu katika machaguo mawili yaliyokuwa halisia:

Serikali 3, Mwalimu alisema ni hofu yake kuwa Muungano unaweza kuvunjika, na yeye hakuwa tayari hilo litokee. Akasema kuwa unapokuwa na Serikali 2, moja ya nchi kubwa kama Tanganyika, na nyingine ya nchi ndogo, pungufu ya wilaya ya Sengerema, ni vigumu muungano wa namna hiyo kuendelea.

Kwenye serikali moja, ambayo ingeifanya Zanzibar, hata kwa upendeleo, kuwa na mikoa labda 2 au 3, Wazanzibari wasingekubali, na huenda wangeona afadhali kujitoa kwenye muungano, na Mwalimu hakutaka kabisa muungano ufe, hata kama wananchi wote wasingeutaka.

Kwa sasa Mwalimu hayupo, mazingira yamebadilika. Tungeweza kuamua kuwa na serikali 1, wazanzibari wasipokubali, tukazanie kuwa na Federation ya East Africa, na Zanzibar iingie humo kama nchi.

Nyerere alikuwa hajiamini kuongoza nchi yake , alitaka kusaidiwa na Wazanzibari na ndivyo mlivyo wengi wa waTanganyika hamjiamini , mpo mpo tu.
Yaani hivi mnavyo andika mnadhihirisha akili zenu zilivyo fupi. Jinchi lenu kubwa lenye kila kitu lakini mnang`ang`ania
kajikisiwa kadogo hiki cha Zanzibar???

Akili ni mali
 
Huenda mwalimu hakuikataa hii hoja ife ni woga wa maccm tu.

Kwa kuona mapungufu ya serikali 2 na historia ya uasi wa mwaka 1984 alishapna hatari mbele lakini asingeweza kukubali kirahisi

Hivyo basi aliwashauri wabunge wale wajitoe ccm ili waunde chama ambocho kingeshinda uchavuzi kwa sera ya serikari 3 na kuunda serikali ya Tanganyika ndani ya muungano

Nyerere alikuwa mjanja sana hakuikataa hoja ife bali alitaka ije kwa njia Ambayo asionekane ni dhaifu
Nyerere hakutaka muungano ufe. Kuna hotuba kali sana aliyoitoa dhidi ya ubaguzi kwa wanaotaka kujitenga. Aliongea kwa jazba sana akitamani “laana” ya ubaguzi iwapate nao wasambaratike; wasibaki wamoja! Clip iko Youtube. Nimeona TBC wakipenda kuirusha siku hizi.

Nilivyoona Nyerere bado alikuwa sentimental sana akipigania legacy yake isifutike kabisa pamoja na ubovu wake. Azimio la Zanzibar lilipopitishwa kufuta Azimio la Arusha alihuzunika sana. Lakini alikuwa smart kujua nyakati zimebadilika. Hakulipigania. Lilipokuja suala la G55 na tishio la kuvunjika Muungano - yeye akiwa hai kushuhudia - aliona, hapana. Akachukua hatua.

Suala la mfumo wa vyama vingi lilipopiga hodi alijua ndio alama za nyakati; halizuiliki. Akaishinikiza serikali ya CCM kukubali. LAKINI hakuwa tayari CCM iondoke madarakani. Alitoa hotuba nyingi za kijanja janja kuhusu katiba na CCM ili kuwaweka sawa watu. Mara CCM si mama yangu, mara kwa katiba hii ningeweza kuwa dikteta mbaya sana, mara upinzani wa kweli utatoka CCM, n.k. Akawatikisa CCM kweli kweli kwenye suala la mgombea wa 1995. Alipompata Mkapa furaha kubwa aliyokuwa nayo ilikuwa dhahiri sana. Alizunguka na Mkapa akimpigia kampeni robust hasa.

Hapo ni kama alisahau kabisa mikanganyiko (controversies) iliyokuwepo kuhusu katiba na muungano. Kumpata “Mr. Clean” aliona kama kamaliza kazi. Kwamba anaweza kurudi Butiama na ku-relax. Hadi aliposhtuliwa na tangazo la mnada wa NBC 😳
 
Nyerere alikuwa hajiamini kuongoza nchi yake , alitaka kusaidiwa na Wazanzibari na ndivyo mlivyo wengi wa waTanganyika hamjiamini , mpo mpo tu.
Yaani hivi mnavyo andika mnadhihirisha akili zenu zilivyo fupi. Jinchi lenu kubwa lenye kila kitu lakini mnang`ang`ania
kajikisiwa kadogo hiki cha Zanzibar???

Akili ni mali
zanzibar ni koloni la tanganyika hatuliachi
 
Msipigige kelele tukiuza mbuga
sisi tunavizia mafuta tu hapo kama wamerekani wala hatuna shida na nyie hata mkitaka wote hamieni huku tunajua hata tukiwapa kawe mnatosha
 
Baada ya miaka 60 ya muungano kuna haja ya kuitisha kura ya maoni baina ya pande mbili ili kila pande iamue kama bado inahitaji kuwepo kwenye muungano!
 
sisi tunavizia mafuta tu hapo kama wamerekani wala hatuna shida na nyie hata mkitaka wote hamieni huku tunajua hata tukiwapa kawe mnatosha

Na sisi tunavizia kuziuza bandari na misitu yenu tu hapo
 
Hawa wajegewe mnara, waliona mbali saana. Ikiwezekana Historiania iandikwe ili watoto ma wajukuu zetu wajue kwamba kuna wakati Bunge letu lilikuiwa na watu makini na wazalemdo wa kweli.
 
Back
Top Bottom