Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.
Kuwa makini haiwezekani wabunge wakatoa kauli ya kijinga kama hiyo eti KUMNASUA na kesi.Masaburi at Work. Peleka Jukwaa la Umbeya au U-turn
Kuwa makini haiwezekani wabunge wakatoa kauli ya kijinga kama hiyo eti KUMNASUA na kesi.
Sikujua kama mtuhumiwa wa mauaji hana haki ya kutetewa.................!
Kumbukeni sio mara ya kwanza lulu anafikishwa kituoni, mara zingine fujo zake zinamkumba hata mama yake; hapo ndo mngekemea tabia hiyo, sasa kuna tukio kubwa tena la kisheria, wabunge makini ningetarajia wangeacha sheria ifute mkondo wake, acheni mambo ya gender gender kwenye suala kubwa kama la kuhusiwa mauaji, hata kama ni kwa bahati mbaya, mahakama itajua.
Mods ondoeni hizi... Maana mimi nimewasikiliza hawa wabunge wanachokisema kiko sawa.
Tatizo lako ni Kufikiria kwa Makalio ambayo hayajatawazwa watu watarajie nini kutoka kwako? Fikra pumba zenye harufu ya Chooni?
Ungeweka Maneno ya Wabunge, Ungeweka ni kwa namna gani wataathiri mwenendo wa Kesi na Ungetuambia ni kwa nini Lulu hastahili watetezi.
La Sivyo Katawaze ili fikra zako zitakaswe
Sikujua kama mtuhumiwa wa mauaji hana haki ya kutetewa.................!
kisheria wenye kesi za mauaji wote hupangiwa mawakili wa utetezi bure,mtuhumiwa ana haki ya kuongeza wake,kwa sasa hahitaji msaada wa kisheria kwa kua kesi haijaanza rasmi,itaanza mahakama kuu atakaposhtakiwa rasmi,tena anaweza asishtakiwe kbs.kumbuka dito alishtakiwa kwa mauaji isivyo rasmi kisutu,badae kuua bila kukusudia rasmi mahakama kuu na kupewa dhamana mawakili wanahitajika hapo. mie nafkiri mdee na huyo mwenzie wangeshughulika kutafuta wabakaji(wapenzi) wa huyo mtoto wawafungulie kesi tofauti.kisheria walikua wanambakaNinavyofahamu mimi Mh. Halima Mdee ni mwanasheria. Kuhusu sakata la LULU (Elizabeth), pamoja na yote yanayozungumzwa bado anahitaji usimamizi wa kisheria ni haki yake. Tunaamini Mh. Mdee ama Mh. Bulaya hawawezi pindisha sheriakama Lulu atakutwa na kosa la mauaji kwa kukusudia. Pia kama itadhihirika kuwa anaumri wa miaka 17 (ingawa najua alishajitangaza na kusheherekea miaka18), atahitaji usimamizi na ushauri kama mtoto maana anaweza kuathirika vibaya sana na pressure ya jambo hili. Tunaamini akipata usimamizi na usaidizi wa kisheria, na kama atahukumiwa kwa kisa la mauaji, basi itakuwa haki imetendeka. Tusipende kukimbilia kuhukumu, bali nakubaliana bado kunautata mkubwa kwenye tukio hili la kusikitisha ssana.
habari yenyewe ya mwanzisha mada ni nyepesi sana 'kuwa wanataka kumsaidia kisheria' lkn watu humu ndani wanatoa maamuzi utadhani usiku ule walikuwapo live ktk tukio na kuhitimisha kuwa binti alilifanya hilo kwa makusudi.
Mmmh mbona maneno makali namna hiyo mkuu asubuhi yote hii...umeguswa kunako?