Wabunge Kenya wapigana bungeni

abena

Member
Joined
Oct 26, 2016
Posts
40
Reaction score
48
Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bungeni mapema asubuhi.

Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyingine katika uchaguzi wa urais mwaka ujao badala ya utaratibu wa kutumia majumuisho ya computer. .

Baadhi ya wabunge hao walikuwa wakivuja damu kutokana na kipondo toka kwa wenzao wa chama tawala.

Hii si mara ya kwanza kwa wabunge wa Kenya kupigana bungeni. Ni aibu kwa wawakilishi wa wananchi kupigana bila aibu.


Chanzo:
BBC swahili
 
Ndunga zao!!
 
Ngoja niwai home kumcheki citizen TV, NTV nk, nimejaribu kiperuz kwenye website zao sijaona wapi wamepiga, ila wabunge wa upinzani walitoka nje ya Bunge.
Narudi ku comment nikishapata habari kamili, nilichoona kwenye Web zao ni kwamba wapinzani wamejipanga kuingia barabarani ku hold peaceful mass demonstration mwakani tarehe nne.
 
Ukiona wabunge wanapigana bungeni ujue wanapigania haki ya wananchi wao, unapaswa kuwasapoti sio kusema eti aibu, pia na wewe mtoa mada unatakiwa kuwa na aibu kwa kulitumia neno aibu pasipo sitahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…