Wabunge kugawiwa mitungi ya Gesi linaleta ukakasi mkubwa. Je, haiwezi kuwa rushwa au waziri kutafuta kukubalika?

Yale yale ya Jairo...
 
Kama wako bungeni kwa wizi wa kura, ni uadilifu gani unategemea kutoka kwao?
 
Kwanza tujuwe ni mitungi ya gas ya kampuni gani?

Kama ni ya Taifa Gas ni wepesi sana kuelewa hiyo ni kazi ya business genius, Rostam.

Kama imetoka kwa Rostam basi hapi itakuwa amewauzia kwa gharama tu wizara ya nishati au hata kawapa bure. Utajiuliza sababu?

Sababu ni nyepesi sana, "kula uliwe" ukitaka kula ni lazima uliwe. Ni pure business na haina uharamu wowote.
 
Uko sahihi kabisa. Bajeti yoyote ya serikali ikienda bungeni, wabunge wa CCM lazima waiunge mkono. Huwa nashangaa hata watu wakisema eti bunge huwa linatunga sheria. Lakini ukitazama uhalisia ni kuwa sheria zote hutungwa na serikali, na huko bungeni ni rubber stamp tu.
 
Kama SI rushwa na utaratibu uliotumia una ukakasi je tuseme waziri anatafuta simple popularity kwa wabunge kujipendekeza kwa malengo binafsi ya sasa au baadae ?
 
Natabiri itakuwa ni Taifa Gas, usiniulize kwann!.
Aisee je bunge litaacha sera ya ushindani na kupromote kampuni moja, huoni wataingizwa kwenye aibu zaidi, kama mhe waziri alivyoacha majukumu yake na kuwa kama sales market manager wa kampuni Moja ya gas ?
 
So it can be a Rostom again !?
Kuwapa Bure itaongeza ukakasi zaidi na maswali zaidi kwa waziri
madam spika kasema waziri kashatenga hela yake kutoka kwenye Kodi za watz wote na hata Kodi za makampuni mengine ya gas,
Wazungu wanasema no free lunch
Naona Kuna jambo nyuma ya waziri
 
Usifikirie sana kichwa kitaexplode!
Hao wanajuana na hapo wanavunjiana genchi tu.
Kama kweli nia dhati ingekua ni kuhamasisha matumizi ya gesi, wangeshusha bei ya gesi, ni genchi episode mkuu!
ni hayo tu,
 
Kama SI rushwa na utaratibu uliotumia una ukakasi je tuseme waziri anatafuta simple popularity kwa wabunge kujipendekeza kwa malengo binafsi ya sasa au baadae ?
Yeye anajiwekea mazingira ya kugombea urais huko mbeleniz sio zaidi ya hapo.
 
Wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, ukitaka kuwafikai wananchi kwa urahisi unapita kwao. Sijui kwa nini unapata tabu kuelewa jambo rahisi kama hilo. Una mawzo ya kizikizi tu na kama watu wanavyo sema kama unakijua basi uanacho au unakifanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…