Wabunge mbona hawakujiajiri?

Wabunge mbona hawakujiajiri?

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,358
Reaction score
10,976
Hawa waheshimiwa wakati wa kunogesha mada mjengoni hutupia kibwagizo cha Watu kujiajiri Ila wao wapo kwenye Payroll miaka na miaka (na mikopo wanachukua benki kwa udhamini wa ofisi) wakiumwa hata mafua tu haoo India miezi 8 bill kwa mwajiri. Akifa jeneza gharama ya mwajiri pia. Imekaaje hii?
 
Hawa waheshimiwa wakati wa kunogesha mada mjengon hutupia kibwagizo cha Watu kujiajiri Ila wao wapo kwenye Payroll miaka na miaka (na mikopo wanachukua benk Kwa udhamini wa ofisi) wakiumwa hata mafua tu hapo India miezi 8. Imekaaje hii?
Wamejiajiri kwenye "Mgodi wao" uliopo kule Dodoma, kweli wewe hujui hili?
 
Hawa waheshimiwa wakati wa kunogesha mada mjengon hutupia kibwagizo cha Watu kujiajiri Ila wao wapo kwenye Payroll miaka na miaka (na mikopo wanachukua benk Kwa udhamini wa ofisi) wakiumwa hata mafua tu hapo India miezi 8. Imekaaje hii?
Ukoo wa kifalme unahitaji kujiajiri? Wakujiajiri kwenye kilimo na ufugaji au biashara za kimachinga na kuendesha toyo ni watoto wanyonge.
 
Ubunge ni kujiajiri ndio maana wajanja wachache tu wenye kipaji cha kujiajiri wameweza kuingia huko. Wanagawana faida kadri wawezavyo-mshahara, posho na mafao wanajipangia. Hivyo wako sahihi kabisa kuwaambia vijana wajiari na fursa ni nyingi sana Tanzania. Wajinga hawawezi elewa mbunge, waziri na hata rais anapohimiza kujiajiri-amka ingia hata kwenye siasa kwani nayo ni ajira
 
Dodoma kila bar na hotel ukiulizia unaambiwa ya mbunge fulani, wakisema wamejiajiri wako sahihi
 
Hawa waheshimiwa wakati wa kunogesha mada mjengon hutupia kibwagizo cha Watu kujiajiri Ila wao wapo kwenye Payroll miaka na miaka (na mikopo wanachukua benk Kwa udhamini wa ofisi) wakiumwa hata mafua tu haoo India miezi 8 bill kwa mwajiri. Akifa jeneza gharama ya mwajiri pia. Imekaaje hii?
Mkuu Chukua form ugombee ubunge 2025.
 
Siyo wote. Wapo baadhi walijiajiri kisha wakapata ukwasi uliowapatia nguvu ya kuhonga wajumbe halafu wakapata ubunge.

Mfano:-
*Kishimba.
*Maganga (wa Jimbo la Mbogwe).
*Msukuma (huyu siyo mfano mzuri, alikuwa mtekaji wa mabasi).
*Aboud wa Morogoro
*Shabiby wa Gairo.
N.k
 
Hawa waheshimiwa wakati wa kunogesha mada mjengoni hutupia kibwagizo cha Watu kujiajiri Ila wao wapo kwenye Payroll miaka na miaka (na mikopo wanachukua benki kwa udhamini wa ofisi) wakiumwa hata mafua tu haoo India miezi 8 bill kwa mwajiri. Akifa jeneza gharama ya mwajiri pia. Imekaaje hii?
Wangejiajiri mngewakilishwa na nani?
 
Back
Top Bottom