Uchaguzi 2020 Wabunge mmemaliza muda wenu msirudi Dodoma kupiga mizinga. Pesa zenu ziwekeze mzalishe ajira; msizitumie kwenye rushwa ya kuomba kura

Uchaguzi 2020 Wabunge mmemaliza muda wenu msirudi Dodoma kupiga mizinga. Pesa zenu ziwekeze mzalishe ajira; msizitumie kwenye rushwa ya kuomba kura

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
wana JF

Haya sasa mshapewa chenu, sasa tunataka kuona mahubiri yenu mliyokuwa mnatuhutubia kuhusu ajira , kilimo kwanza, viwanda. tayari mtaji wa kuwa na viherani saba kuwa kiwanda mnazo hela. Sisi wasio na kazi tunangoja hela zenu zitutengenezee ajia. Muigeni Mh. Pinda anafuga Nyuki, anafuga Ng'ombe.

Lakini kumbukeni kura za maoni ni mwanzo wa vifo hutokea maana ukimwaga vibaya mahela alafu ukakatwa ndio mwanzo wa mawazo. mwanzo wa umaskini unakukaba unaanza kwenda kuomba kwa wabunge wenzio. huku ndio kuitwa ombaomba.
 
Siasa ni kama kuchimba madini,wachimbaji wakipata mamilioni, wanatanua alfu baada ya muda wanafulia wanarudi tena kuchimba.
 
Siasa ni kama kuchimba madini,wachimbaji wakipata mamilioni, wanatanua alfu baada ya muda wanafulia wanarudi tena kuchimba.
bora pesa hizo sasa wakafugie kuku, nyuki wazalishe ajira sio kuzitafuna na vimwana alafu waje kupiga mzinga
 
wana JF

Haya sasa mshapewa chenu, sasa tunataka kuona mahubiri yenu mliyokuwa mnatuhutubia kuhusu ajira , kilimo kwanza, viwanda. tayari mtaji wa kuwa na viherani saba kuwa kiwanda mnazo hela. Sisi wasio na kazi tunangoja hela zenu zitutengenezee ajia. Muigeni Mh. Pinda anafuga Nyuki, anafuga Ng'ombe.

Lakini kumbukeni kura za maoni ni mwanzo wa vifo hutokea maana ukimwaga vibaya mahela alafu ukakatwa ndio mwanzo wa mawazo. mwanzo wa umaskini unakukaba unaanza kwenda kuomba kwa wabunge wenzio. huku ndio kuitwa ombaomba
Daaa. Hivi wamelipwa ngapi?
 
Zilifaa kuchelewa mwaka mzima kama wastaafu wengine ili kupunguza na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu.
 
Mtu aliyezoea kuajiriwa ni vigumu sana kumwambia aanze kufikiria kujiajiri, wengi ni waoga na wanaamini hawawezi. Ilà kwa mpunga wanaopata ndani ya mda mfupi(miaka mitano) mtu unaweza kujiajiri kabisa na maisha yakawa safi tu.

Hivi wakiingia mjengoni wanakopeshwa ili kununua gari gani?
 
Back
Top Bottom