Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hakuna kitu cha kuangalia sana kama mwitikio wa watawala wakati wa dharura. Kwani ni wakati huo ambapo watawala wanahisi kuwa wanaweza kupitisha jambo lolote lile kwa kisingizio cha "dharura". Katika nchi ya kidemokrasia ambayo msingi wake ni sheria, uhuru, uwazi, usawa na kuwajibika (miongoni mwake) ni jukumu la wananchi kuangalia sana kile watawala wanafanya katika wakati wa kawaida lakini zaidi wakati inapotokea dharura.
Alichofanya Rais Kikwete jana ni kitu ambacho endapo kitakumbatiwa kwa haraka na kumezwa bila hata ya kuangaliwa kwa ukaribu tunaweza kujikuta tumeruhusu kitu cha hatari zaidi katika uchumi wetu.
Kwanza, uamuzi wa yeye kutoa pendekezo la matumizi haya makubwa ambayo yana implication nzito sana kwa uchumi wa taifa nje ya Bunge ni uamuzi ambao unanifanya nijiulize kwanini hakutaka kuzungumza na wawakilishi wa wananchi Bungeni.
Huu mtindo wa kuzungumza na "wazee" itabidi siku moja tuukomeshe kwani kama mambo mazito kama haya yanazungumzwa kwa watu ambao moja hawawezi kupewa nafasi ya kujadili kilichosemwa na pili kuzungumza tu kama vile kuwalisha watu chakula bila kuwapa muda wa kunywa maji ni mtindo mbaya.
Kama tukikubali kuwa hali ni mbaya kama Rais alivyoichora kwenye mawazo ya baadhi ya watu kwa karibu theluthi mbili ya hotuba yake basi alichagua mahali pasipo sahihi kufafanua ubaya wa hali hiyo.
Lipo kundi moja tu ambalo kitaifa linawawakilisha Watanzania na pekee limepewa jukumu la kusimamia serikali na kundi hilo haliitwi "wazee wa mkoa fulani". Kundi hilo siyo wakufunzi wa Chuo Kikuu na kundi hilo siyo mashabiki fulani bali ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kuamua kupeleka mapendekezo yake nje ya Wabunge, na kwa kuamua kupigia debe matumizi makubwa kabisa ya serikali wakati wa amani nje ya Bunge, Rais Kikwete amejaribu (naombea bila mafanikio) kulikwepa Bunge na hivyo kuwanyima wabunge haki ya kupitia mpango mzima wa serikali.
NI kwa sababu ninafahamu kuwa Mkullo atakaposimama atakuwa ametengenezewa njia rahisi ya kuleta bajeti hiyo ya matumizi ya serikali na mpango huu wa ajabu.
Natumaini wabunge watasahau yote aliyoyasema Rais Kikwete na kumsikiliza Mkullo na bajeti yake na hicho pekee ndicho kiwe kipimo cha nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na hali ya uchumi nchini. Waipime hotuba hiyo ya bajeti, wachuje matumizi yasiyo ya lazima na ikibidi watungie sheria ya kushughulikia suala hili la matatizo ya kiuchumi badala ya kujaribu kuliingiza ingiza kwenye mipango mbalimbali kama nyongeza na mwisho wake kutengeneza mchezo wa kupoteza mabilioni ya fedha ambayo ni kawaida ya serikali.
Wakati huu wa dharura; wabunge wetu ndio wanatakiwa kusimama kama kinga ya mwisho dhidi ya ubabe (the last defense against tyranny) wa serikali.
Cheche wiki hii itachambua mapendekezo haya ya Rais na kuyaonesha ni kwanini kwa maneno mawili ni "wizi mtupu"! Ni mapendekezo ya mtu maskini ambaye anajifikiria ni tajiri kwa vile ati anaweza kukopa na hivyo kuanza kupanga matumizi ya kifahari ya fedha za kukopeshwa!
Wabunge, msiburuzwe!