Wabunge na Mawaziri Muungano Mmeishiwa: SMZ

Wabunge na Mawaziri Muungano Mmeishiwa: SMZ

Zanzibar pia ni rahisi kujitoa kwenye Muungano ,tatizo serikali zote mbili wanafadhiliana kukaa kwenye madaraka ,Mgombea kiti cha uraisi .CCM Tanganyika wanategemea Zanzibar na Mgombea Zanzibar anategemea CCM wa Tanganyika.
Ila siku upinzani ukishika madaraka na kuwatolea uvivu mafisadi ni lazima ikubalike kuwa kunahitajika ukarabati wa haraka wa Muungano au mkataba mpya la sivyo patagawanywa mbao.

Well said Mwiba.
Ni mpaka hapo CUF wakichukua madaraka ya Urais Zanzibar, (au hata Chadema Tanganyika) ndiyo muungano unaweza kuvunjika (By the way, haitakuwa kitu kibaya, kwani inaonekana kila upande unadhani unakosa haki kuwa ndani ya Muungano).

Hii ndio inafanya CCM kuendelea kung'ang'ania madaraka by hooks & crooks. CCM wa pande zote mbili wanategemeana kubakia madarakani. Si mnakumbuka isingekuwa CCM-Tanganyika ni Dk. Bilali ndiye angekuwa anayemalizia urais Zanzibar, siyo Bw. Karume?
Na CCM-Zanzibar ilimbeba sana Kikwete kwenye mchakato ndani ya CCM...

Yote yanayotokea nchini kwa sasa (na response ya Serikali ya Muungano) yanaleta tena questions about leadership capability ya Mkuu wa sasa...
 
Che Guavara,

..ninavyoelewa mimi mtandao ndiyo walimuwezesha Karume kumshinda Bilali kule Dodoma.

..Karume naye akawalipa kwa kumsaidia Kikwete dhidi ya Mzanzibari mwenzake Salim Salim.

..ungetegemea kwamba serikali ya Kikwete na ya Karume wangekuwa na maelewano kuliko inavyoonekana sasa hivi.

NB:

..binafsi nadhani Muungano huu hauwezekani kwasababu Tanganyika ni kubwa mno kuliko Zanzibar. hatuwezi kukaa tukaelewana as equal partners wakati ratio ya wananchi wetu ni 1:36.

..vilevile, wakati Watanganyika tumekubali na tunajivunia kuwa Watanzania, wenzetu Wazanzibar wameweka mgomo kuuacha utaifa wao.

..
 
Ni mpaka hapo CUF wakichukua madaraka ya Urais Zanzibar, (au hata Chadema Tanganyika) ndiyo muungano unaweza kuvunjika (By the way, haitakuwa kitu kibaya, kwani inaonekana kila upande unadhani unakosa haki kuwa ndani ya Muungano)
Kwani chadema na wao wanataka serikali tatu!
Sera zao kuhusu muundo wa muungano inasemaje?
 
Che Guavara,

..ninavyoelewa mimi mtandao ndiyo walimuwezesha Karume kumshinda Bilali kule Dodoma.

..Karume naye akawalipa kwa kumsaidia Kikwete dhidi ya Mzanzibari mwenzake Salim Salim.

..ungetegemea kwamba serikali ya Kikwete na ya Karume wangekuwa na maelewano kuliko inavyoonekana sasa hivi.

NB:

..binafsi nadhani Muungano huu hauwezekani kwasababu Tanganyika ni kubwa mno kuliko Zanzibar. hatuwezi kukaa tukaelewana as equal partners wakati ratio ya wananchi wetu ni 1:36.

..vilevile, wakati Watanganyika tumekubali na tunajivunia kuwa Watanzania, wenzetu Wazanzibar wameweka mgomo kuuacha utaifa wao. ..

Maelewano yapo tena ya kishindo si unaona hao wezi wa kura wanavyopelekwa Pemba ? Hizi kelele zisikupe tabu sana ni nyimbo tu za danganya toto watu kutoleana mijicho kumbe ni tactics za kuupoteza umma. Serikali ya Zanzibar inajua wazi kuwa kama Serikali ya Kikwete itatupa manyanga na kuweka mkwala wa kufanyika uchaguzi wa haki Zanzibar basi SMZ itaambulia chini ya robo ya robo ya kura za Zanzibar au kura zisifike hata elfutano ,hilo linaeleweka wazi kabisa wala halina mjadala.

Na WaZanzibar wanafahamu namna game hii inavyochezwa ila wanasema itakavyopigwa ndivyo itakavyochezwa.
 
Che Guavara,

NB:

..binafsi nadhani Muungano huu hauwezekani kwasababu Tanganyika ni kubwa mno kuliko Zanzibar. hatuwezi kukaa tukaelewana as equal partners wakati ratio ya wananchi wetu ni 1:36.

..vilevile, wakati Watanganyika tumekubali na tunajivunia kuwa Watanzania, wenzetu
sasa liangalie hilo katika jicho la uchambuzi. Hiyo ratio yako hiyo. Hivi mkisema mmekubali kuacha utaifa wenu, enhe!! unaachika hapo? sasa na kwa nini sisi -angalia ratio hiyo tusin'gan'ganie utaifa wa wetu (Nyinyi achieni sisi tutan'gan'gania daima). Uzanzibari umeimarika sasa. Na ninashukuru hata watoto wetu wa Maandalizi (kwenu mnaita chekechea). Ukimuuuliza kwanza anakueleza kwa ufasaha yeye ni Mzanzibari.
 
Na WaZanzibar wanafahamu namna game hii inavyochezwa ila wanasema itakavyopigwa ndivyo itakavyochezwa.
Hivi wanaokushindeni katika kura ni watu wa Kikwete walioko Bara au Wazanzibari wenzenu walioko huko huko kwenu Zanzibar? Usituzingue Bwana. Leta hoja yenye meno.
 
Kwani chadema na wao wanataka serikali tatu!
Sera zao kuhusu muundo wa muungano inasemaje?
Nafikiri kwa sababu na wao pia wana mawazo ya kuvunja Muungano- nazungumzia Muungano ule uliofikiwa 26/1964, ambao CCM imejizatiti kuuendeleza kwa faida na manufaa ya pande zote mbili.
 
Kwa nini tusifanye referrendum na kuamua for good kama huu muungano unaendelea au la?
 
Kwa nini tusifanye referrendum na kuamua for good kama huu muungano unaendelea au la?

That is the best option. Lakini since ni referendum kuhusu two countries lazima ifanyike moja kwa wabara na nyingine kwa wazenji then tukubaliane kuwa kila nchi lazima idadi fulani ya wananchi wakubali ndiyo muungano uendelee. Ina maana kama any of the sides hawata pata hiyo asilimia then hakuna muungano. But that will require kuweza kutambua kihalali nani mzenji na nani mbara. Is there are way of knowing that? Na pia kuna swala la kama referendum itakuwa huru na ya haki.
 
Teh teh si waachiwe tu mi nashangaa why tuwabebe tu wazushi hawa? mbona umeme wetu watumia kwa bei ya bure kabisaa, kwetu kwao kwao kwao waende bwana.
 
Kwa nini tusifanye referrendum na kuamua for good kama huu muungano unaendelea au la?
Kwani mlipoanzisha Muungano mlifanya hiyo referendum. Iweje muitake sasa? Hilo haliingii akilini.
 
Kwani mlipoanzisha Muungano mlifanya hiyo referendum. Iweje muitake sasa? Hilo haliingii akilini.

Mkuu that's not a very compelling argument. Hauwezi kusema kwa sababu tu kitu hakiku fanyika wakati fulani basi kisifanyike. Kwa mawazo yangu there should have been a referendum in the first place kabla ya kuungana. Tatizo siasa za wakati huo ilikua chochote raisi anacho taka ndicho anacho fanya bila kujali wananchi wana taka nini. Is that what you want?
 
Nakuelewa vizuri na suala la referendum. Hata mimi ningetaka ifanyike hapo mwanzao. Lakini haikufanyika. Hivyo la sasa Muungano ndio upo hakuna haja kurudi nyuma kufanyahivi referendum. Lakini ni kuwasikiliza wale ambao hawakupata fursa ya kusema kuhusu kuanzishwa Muungano huo, ni vipi wanataka uendeshwe ili kukidhi maslahi yao.
 
Kwanini siku zoote Watu wa upande mmoja wanakuwa wako sawa na wengine wako wrong daima
Lakini hawaya mmezoea kufanyiwa kila kitu sasa leo mna tapatapa, kama upinzani ndio ulio sema hivyo basi nyinyi wanafiki wa kizenj mtakanusha na kulaani kweli kweli lakini mimi ninasema mzee sitta na hata baado.
 
Nafikiri kwa sababu na wao pia wana mawazo ya kuvunja Muungano- nazungumzia Muungano ule uliofikiwa 26/1964, ambao CCM imejizatiti kuuendeleza kwa faida na manufaa ya pande zote mbili.
Pakacha, chadema katika hili naona kama wanafiki wanafiki hivi, matendo yao hayaonyeshi kuwa wanataka Muungano bora nimeshuhudia baadhi ya wajumbe wao wakikejeli mawazo kama hayo.
Halafu Pakacha, mpaka leo hujaelewa tu kuwa Muungano haukuafikiwa bali umeshinikizwa? na mpaka leo hujaelewa kuwa muungano huu haupo kwa manufaa ya pande mbili bali kwa watu wachache tu wanaigeuza zanzibar kama shamba la bibi tu, wao wanavuna tu hawachangii mbolea wala nguvu za kulimia?

Hivi wanaokushindeni katika kura ni watu wa Kikwete walioko Bara au Wazanzibari wenzenu walioko huko huko kwenu Zanzibar? Usituzingue Bwana. Leta hoja yenye meno.
Ni mamluki kutoka bara wanaopelekwa zanzibar katika kila kipindi cha uchaguzi. Na hivi sasa wapo mbioni kupeleka mamia ya askari Zanzibar katika muda ambao zoezi la uandikishaji linaanza kuelekea uchaguzi mkuu.
Badao wale waliokwisha tanguliza katika makaazi ya watu na kupangishwa majumba ya mji mkongwe. Wapo watakaoletwa kwa majahazi siku ya uchaguzi mkuu. Kuna mambo!!!

Teh teh si waachiwe tu mi nashangaa why tuwabebe tu wazushi hawa? mbona umeme wetu watumia kwa bei ya bure kabisaa, kwetu kwao kwao kwao waende bwana.
Ndugu yangu ww ukiwa na mawazo hayo wenzako wanatazama akaunti zao zitakuwaje kama mirija yao ya unyonyaji itakapo katwa zanzibar?
Na umeme kwa taarifa yako hautumiki bure zanzibar wanalipa na ww huna ushahidi wwte kuwa wanatumia umeme bure.
 
SMZ wanaotikisa nguzo za muungano ni walevi wa madaraka na wanaona wakisimamia hoja hiyo ya kudai mafuta na gesi asilia ambayo bado ni hekaya watabakia ktk nafasi zao. Ila hawajui kwamba maadui wa muungano wameshawasoma udhaifu wao na wameenda mbele kuwatega ambapo sasa wanaingia kiulaiiin ili wavunje muungano na zenji iingie ktk trauma.

Miaka yoooote wanakula mali ya uma na hawapeleki maendeleo kunakohusika halafu leo wanakuja na machozi ya mamba wakidai wanatetea zanzibar. Hawa viongozi hawana chembe ya utaifa na uzalendo wa Kitanzania ambapo waliapa kuilinda na kuitetea ila sasa wameamua kuunda ajenda ya siri wakiamini wako sahihi. Hawa nawaita viongozi maruhani ambao kwao kulinda maslahi yao ni thamani kuliko uhai wa wananchi wao.

Ni wapuuuzi na wanapaswa kupuuzwa kama vibaraka wengine wowote. Ila mie namlaumu kikwete kwa kuwa mjomba mno kwa ishu za maana kama hizi. and huyo mshauri mwelekezi wa mafuta alishawahi kuapa kuwa atailinda na kuitetea katiba ya tanzania????? Gademu
 
Back
Top Bottom