Kuna Mamlaka mbili zinazosimamia barabara za Mikoa na barabara za Vijijni(Halmashauri). Mamlaka hizi zinagawiwa fedha na Serikali kila mwaka kutekeleza kazi za barabara kwa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara.
Nitoe mfano. Awamu ya nne kabla ya kuanzishwa TARURA ujenzi wa barabara ulikuwa unasimamiwa na Halmashauri lakini katika awamu ya tano ukaanzishwa TARURA yaani TANZANIA RURAL ROADS AGENCY. Wakati wa awamu ya nne kwa wastani kila Halmashauri ilikuwa inagawiwa wastani wa Tshs 800,000,000 kila mwaka ingawaje walikuwa na matatizo katika utekelezaji wa majukumu yao lakini katika awamu hii ya tano chini ya TARURA Halmashauri hupewa wastani wa Tshs 300,000,000 kutekeleza kazi zote za ujenzi wa barabara katika Halmashauri wakati TANROADS wanapewa wastani wa Tshs10bn kwa mwaka. Tujiulize wapi kuna watu?
Natumaini vijijini ndiyo kuna watu. Tukumbuke kuwa mwaka huu kumekuwa na uharibifu mkubwa wa barabara katika maeneo ya vijijini.
Je, Tshs 300,000,000 inaweza kutosha kwa Halmashauri kwa uharibifu huu wa barabara zetu vijijini? Pili, kwa nini rate ya matengenezo ya barabara za Tanroad na TARURA ni tofauti? Mfano kutengeneza kilomita moja ya barabara ya Tanroad na TARURA kiwango cha TARURA kiko chini sana.
Waheshimiwa Wabunge, pazeni sauti zenu ili TARURA wangezewe fedha za matengenezo za barabara na ni wakati mzuri mko kwenye vikao vya Bunge.