Bunge la Wananchi
Member
- Jan 30, 2023
- 16
- 14
Wabunge wa Mkoa wa Simiyu wamesusia kongamano lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kihongosi kwa lengo la kuunga mkono Azimio la Mkutano Mkuu kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais mwaka 2025.
mkutano huo umefanyika wilaya ya Bariadi ambapo hata mbunge jimbo husika la Bariadi hakuhudhuria kongamano hilo lililoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu KIhongosi.
Hata hivyo kwenye kongamano hilo ni mbunge mmoja tu wa Itilima, Njalu Silanga ndiye aliyehudhuria na kuacha maswali mengi kwa wananchi waliohudhuria kongamano hilo kwanini wabunge wasususie kusanyiko hilo?
Baadhi ya makada wa CCM wamedai sababu za wabunge hao kususia kusanyiko hilo ni kwamba tayari mkutano mkuu wa ccm ulishafanya kazi yake Dodoma na kuhoji nini mantiki ya kuanza tena kampeni hizo ngazi ya mkoa?
Wana CCM hao wameuomba Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee Wasira kumchunguza mkuu wa mkoa wa simiyu kwanini anatumia fedha nyingi za umma kujiingiza kwenye makundi ya kisiasa badala ya kufanya kazi alizotumwa za kusimamia maendeleo ya wananchi wa mkoa wa simiyu.
Hata anapotengeneza clip za kujifanya anamsifia rais Samia ukifuatilia commments nyingi kwenye istagramu yake utagundua wanaomsifia ni watu wa nje ya Simiyu wengi ni marafiki na viongozi wenzake walioko Dodoma, Iringa, Arusha na Dar na sio wananchi wa mkoa wa simiyu anaowaongoza na yote anajitetea ili asitumbuliwe kutokana na usimamizi wake mdogo wa shughuli za maendeleo mkoani simiyu.
Wakurugenzi wa halmashauri nyingi za Simiyu wanafuja fedha wanashirikiana na baadhi ya madiwani miradi haikamiliki lakini ukimsikiliza mkuu wa mkoa utadhani anafanya kazi kumbe usanii mtupu ndio sababu alishindwa kazi hadi akaondolewa UVCCM kama katibu mkuu leo atawezaje kuongoza mkoa tena wenye changamoto nyingi kama simiyu.
Kazi kubwa anayoifanya yeye Kihongosi ni kukanusha tu taarifa kwamba mkoa wake hakuna matatizo kwenye sekta ya elimu shule zote zina miundombinu ya kutosha hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa madawati mkoa mzima, shule zina vyoo vya kutosha, nyumba za walimu na kwamba mkoa wa simiyu hauna matatizo yoyote kwenye sekta ya elimu