Wabunge Subira Mgalu na Saasisha Mafuwe wampongeza Mchengerwa bungeni kwa Kasi ya Maendeleo

Wabunge Subira Mgalu na Saasisha Mafuwe wampongeza Mchengerwa bungeni kwa Kasi ya Maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu, ametoa pongezi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa (MB), kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta suluhisho ya changamoto za wananchi na kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaendelea kwa kasi na ufanisi katika maeneo mbalimbali nchini, hususan mkoani Pwani.

Mhe. Mgalu amesema juhudi za serikali kupitia TAMISEMI zimeleta matokeo chanya, hususan katika sekta ya miundombinu ambapo barabara za vijijini na mijini pamoja na madaraja makubwa na madogo zimeendelea kujengwa kwa kiwango kikubwa.

Mhe. Mgalu Amepongeza ujenzi wa Daraja la Muhoro, wilayani Rufiji, linalojengwa kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kuwa ni miongoni mwa miradi muhimu inayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa eneo hilo na mkoa kwa ujumla.

Vilevile Mbunge Saasisha Mafuwe, amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kwa kazi nzuri na ya kizalendo anayoifanya katika wizara hiyo.

Mheshimiwa Mafuwe amesema kuwa Waziri Mchengerwa ameonesha uongozi wa mfano kwa kusimamia vema shughuli za maendeleo na huduma za kijamii, pamoja na kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ikiwemo Jimbo la Hai. Ziara yake katika jimbo hilo imeleta matumaini mapya kwa wananchi na kuashiria dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania.

“Waziri Mchengerwa ni mtu wa kazi. Uwepo wake Hai na ushiriki wake kwenye masuala ya kijamii unaonesha jinsi alivyojitoa kwa wananchi. Hongera sana kwa kazi nzuri na moyo wa kizalendo,” amesema Mhe. Mafuwe.

 

𝐌𝐈𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐎 𝐘𝐀 𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 𝐁𝐀𝐉𝐄𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐌𝐈𝐒𝐄𝐌𝐈 2025/26

" 𝐇𝐀𝐊𝐈𝐊𝐀 𝐌𝐂𝐇𝐄𝐍𝐆𝐄𝐑𝐖𝐀 𝐖𝐄𝐖𝐄 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐙𝐈" - 𝐌𝐇𝐄. 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐖𝐄
​

Mbunge wa Jimbo la Hai, Mheshimiwa Saasisha Mafuwe, amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kwa kazi nzuri na ya kizalendo anayoifanya katika wizara hiyo.

Mheshimiwa Mafuwe amesema kuwa Waziri Mchengerwa ameonesha uongozi wa mfano kwa kusimamia vema shughuli za maendeleo na huduma za kijamii, pamoja na kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ikiwemo Jimbo la Hai. Ziara yake katika jimbo hilo imeleta matumaini mapya kwa wananchi na kuashiria dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania.

“Waziri Mchengerwa ni mtu wa kazi. Uwepo wake Hai na ushiriki wake kwenye masuala ya kijamii unaonesha jinsi alivyojitoa kwa wananchi. Hongera sana kwa kazi nzuri na moyo wa kizalendo,” amesema Mhe. Mafuwe.

#𝑴𝒄𝒉𝒆𝒏𝒈𝒆𝒓𝒘𝒂𝑴𝒕𝒖𝑲𝒂𝒛𝒊
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-04-18 at 01.10.43.mp4
    4 MB
Uchaguzi SM 2024 alifanya kazi nzuri sana

No Reforms, No Elections!
 
Back
Top Bottom