Wabunge, TUCTA, watu hawajalipwa mpaka leo, mmechukua hatua gani?

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
1,470
Reaction score
515
Najiuliza, hawa ndugu zetu waheshimiwa mbona hatuwasikii mkitetea wananchi wenu? Inawezekanaje mpaka leo tar 37 watu hawajalipwa na mmekaa kimya? au kwakuwa posho zenu zinaflow kama kawaida? na nyinyi Tucta ndo nini kukaa kimya? au kwakuwa watumishi wa umma ni laki tano tu? Mgimwa hajaona umuhimu wa kutoa statement, hata nyie? Tanzania bwana, ajabu kabisa.
 
Kumbe chaguzi za CCM zilichotewa kiasi kikubwa sana cha pesa za umma !!!
 
Tanzania kuna tatizo kubwa katika mfumo wa vyama vya wafanyakazi! Kwanza hii kazi haipaswi kuwa ya wabunge, wabunge ni secondary ila vyama vya wafanyakazi ndio majukumu yao haya! Nilishangaa sana wakati ule wa ishu ya mafao ya kujitoa nio wabunge wawili ama watatu tu waliokomalia kweli kweli huku vyama vingi vya wafanyakazi vikiwa kimya( isipokua TAMICO) kama sijakosea hilo jina ila ni kile chama cha wafanyakazi wa midodini ndio kidogo waliongea.

Sasa na hili limekuja watu wamekopwa nmpaka leo Trade Unions wako kimya sijui nao washashikishwa bahasha?
 
Jamani hii sio haki kabisa kama mpaka leo hamjalipwa vijisenti Serikali inabidi iwajibike!
 
Hata mimi sijalipwa mshahara hadi leo na hakuna taarifa zozote zinazoelezea ni kwa nini waumishi wa umma hawajalipwa mshahara hadi leo tarehe 38. Nyerere alikwisha sema serikali corrupt haikusanyi kodi. Hukimbizana na watu wadogo huku wafanyabiashara wakubwa wakiachwa! Hali hii imejitokeza sasa! TUCTA mko wapi au mmeshakula chenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…