Wabunge viti maalumu ni mzigo kwa Taifa

Wabunge viti maalumu ni mzigo kwa Taifa

Lyetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
1,404
Reaction score
3,748
Bunge la Tanzania lina zaidi ya wabunge 100 wa viti maalumu. Hawa watu mchango wao ni upi kwa Taifa? Nikweli nchi yenye uchumi wa chini kama Tanzania tunahitaji kurundika watu wote hao bungeni?

Ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, idadi hiyo ipunguzwe hadi idadi ya wabunge wa viti maalumu 50.

Nafasi hizo 50 zinazopaswa kuwa za viti maalumu ziwe nikwajili ya maexpert tu kwenye nyanja tofauti kama Afya, Nishati, Sheria, Teknolojia n.k ili waweze kushauri, kutunga sera na kuikosoa serikali kwenye mambo ya kitaalamu.

Uwakilishi wa wanawake kupitia ubunge wa viti maalumu ufutwe mara moja, tayari tunayowizara na Sheria zinazolinda haki za mwanamke. Mwanamke anaehitaji ubunge apite kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa majimbo.

Bunge sio sehemu ya kujaza watu wajinga wajinga tu wanaokula pesa za bure na hakuna chochote wanalisaidia Taifa eti tunatengeneza usawa wa kijinsia.

Wabunge 10 wanaoteuliwa na Raisi wafutwe, idadi ya wataalamu 50 wanaopaswa kuwa wabunge wa viti maalumu wanatosha kuishauri serikali.

Wabunge hawa 50 wataalamu wa mambo mbalimbali ambao watakuwa wabunge wa viti maalumu wapatikane nje ya mfumo wa siasa.
 
Wabunge kutoka Zanzibar nao ni mzigo tu kwenye bunge la Tanganyika. Hawana faida wala tija yoyote. Wabakie kwenye baraza lao la wawakilishi.
 
Back
Top Bottom