Hivi kweli huyu Makamba ni wa kumpigia debe kwa kejeli namna hii? Eti inafikia hatua baadhi yenu mnadai sasa Msambaa kapewa zigo na amelifikisha hii ni kebehi kubwa.
Mpaka sasa nishati ya umeme ni tatizo hapa nchini. Maana kila siku ni umeme kukatika hovyo.
Tangu awe waziri ni harufu ya ufisadi na ujanja tu ndani ya hii wizara ya nishati. Ukarabati wa miundo mbinu usiokwisha na kandarasi za kijanja kijanja kama ya Mahindra Tech. Lakini hakuna tija kwa wananchi.
Inashangaza sana kuona wabunge mnasifia upuuzi huku wananchi wakiumia kwa kukosa nishati ya uhakika huku bwawa la JNHP likidorola kwa sababu za ajabu ambazo ni upigaji pesa wa kiroho usio na huruma kwa raia.