Wabunge wa CCM mbona mnafeli sana kwa Mbowe?

Wabunge wa CCM mbona mnafeli sana kwa Mbowe?

Kwa hali ilivyo ni dhahiri bunge hili la mwisho la Ndugai, bila kupenda litakuwa linajadili hotuba ya jana ya Mbowe kuhusu Corona hadi litakapovunjwa rasmi 30/6/2020

Wabunge wa CCM mara nyingi wamekuwa na udhaifu wa kutegeka kirahisi na mitego ya Mbowe na hili halina afya kwa bunge, chama wala mbunge mwenyewe binafsi bali ni kumpa KIKI huyo Mbowe.

Kwanini umjadili Mbowe wakati kuna mambo mengi ya msingi ya kujadili na muda wenyewe ni mchache?

Mwacheni Mbowe na pumba zake nyie fanyeni kazi tuliyowatuma, kumpayukia huyo Mbowe hakuna msaada wowote wa wewe kurudi bungeni October.

Maendeleo hayana vyama!
Hii atakuwa amekupa mzee Mgaya. Maana ina uzito ndani yake.
 
Umeanza matusi si vema kwa mtu kama wewe ingawa sikujui! Futa hilo neno please. Wewe humu una kaheshima kiasi fulani!
Hao wabunge wa chama changu ndio wanadai hotuba ya Mbowe imejaa pumba tupu, siyo mimi bwashee!
 
Mbowe anatafuta umaarufu wa kisiasa tu

Unajua Kwanini Mbowe anataka lockdown yeye kwa mwezi analipwa na serkali zaidi ya milion ishirini kwa mwezi Kwahiyo Wewe mwanambagala hata ukifa njaa Mbowe hana habari
Hahahahahaha acha kuchekesha, Mbowe atafute umaarufu wa kisiasa?? Mbona walioji-lockdown chattle na wanalipwa hata zaidi ya Mbowe huwataji?? Unafiki kwa mtoto wa kiume mbaya sana
 
Hawa mbwa watetea serikaki badala ya wananchi wananikera sanaaa
 
Tangu lini wabunge wa Ccm wakawa na uwezo wa kujadili hoja za msingi bungeni? Wanachoweza wao ni kupiga meza, kupiga vigeregere, kuunga mkono hoja, kuitikia 'ndiyoooooo', kuwapiga vijembe wapinzani, kutumia muda wao kupongeza badala ya kuelezea changamoto za majimbo yao , nk.

Nitasikitika sana iwapo wabunge wengi makini wa upinzani hawatarudi kwenye bunge lijalo, maana binafsi nitakata kabisa tamaa ya kuangalia vioja vya wabunge wa ccm.
mbunge wa maana wa mwisho ccm alikuwa marehemu Filikunjombe, rip
 
Wewe ndo hukitakii mema Chama. Wabunge wa CCM wameambiwa wajitahidi kumjibu Mbowe maana kwenye Chama hakuna mwenye uwezo huo.
Na wanao jaribu kumjibu wana kwenda off point. Ukiwa Ccm lazima uwe kilaza hata kama una PHD unaiacha mlangoni hadi utakapo toka Ccm ndio urudie PHD yako. Kama wale walio okotwa jalalani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wabunge wa chama changu ndio wanadai hotuba ya Mbowe imejaa pumba tupu, siyo mimi bwashee!

..mawaziri wasiwe wabunge.

..raisi asiwe mwenyekiti wa chama tawala.

..kiongozi wa kambi ya upinzani asiwe mwenyekiti wa chama.

..na Spika atoke nje ya bunge.

..hayo yakifanyika yanaweza kusaidia kupunguza utovu wa ni nidhamu tunaoushuhudia bungeni.

..
 
Wamuachie mzee Mgaya!

Back
Top Bottom