Uchaguzi 2020 Wabunge wa CCM mpya ni mkakati maalum wa kubadili katiba, Paul Makonda na Alexander Mnyeti ni kishindo kikuu

Uchaguzi 2020 Wabunge wa CCM mpya ni mkakati maalum wa kubadili katiba, Paul Makonda na Alexander Mnyeti ni kishindo kikuu

Hao wapinzani wa kupeleka bungeni wako wapi ?
Cha msingi mi naona wananchi tuamke tupeleke wabunge wa upinzani wakutosha bungeni, vinginevyo tutakuja kujuta huko mbele. Mungu epusha haya yasitokee
 
Hii ni kweli kabisa kila mwenye akili timamu ameshaona hili taifa linakoelekea,kama hawa watu wataingia bungeni kuanzia januari 2021,hii nchi itabadilika sana!
 
Dalili zinaonekana, mtu kama Musiba anataka kwenda bungeni kufanya nini?!

Amesifia kwenye gazeti lake ameona hiyo haitoshi sasa anataka kupeleka mapambio yake bungeni, hilo bunge lijalo linaweza kuwa la hovyo zaidi ya lile lililopita la Ndugai.
Kila mtu anao uhuru wa kugombea ubunge na kuchaguliwa ikiwa itawafaa wapiga kura. Wewe ni nani mpaka useme huyu anafaa na yule hafai.
 
Tuki fikia uko basi watanzania Tutakua tume kubari kuolewa na CCM
 
Hii iwe funzo kwa waasisi wa katiba mbovu inayompa mamlaka yasiokuwa na ukomo mtu mmoja kwenye nchi.Pia vyama kutokuwa na nguvu ya kumdhibiti rais.
Kwa kweli Tanzania inapitia kipindi kigumu labda Mungu aingilie kati huko mbeleni kwa kupindua meza kibabe.
 
Thats logical bunge likiwa limejaza amateurs ambao hawana uzoefu wa kubishana juu mwelekeo wa chama ata kama wote wasomi Magufuli can do pretty as he pleases akiamua kubadili katiba wala sio issue.

Hila kubadili katiba ya nchi ni jambo moja na kubadili katiba ya CCM ni jambo jingine na huku ndio kuna amua upate ridhaa ya kuendelea ata yeye Magufuli atakuwa anajua hii ni mission impossible ndani ya CCM.
Hata wakibadili katiba kwa kumlenga mtu na ulafi tu hawataweza kuongeza miaka ya kuishi. Wakifanya hivo future yao itajakuwa ni mateso na kilio na kusaga meno. Haihitaji akili nyingi kujua hili.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hata Bunge zima liunge mkono hoja ya kuongezewa muda rais ,huku kitaani hatutokubali hata iweje,kama anataka kujiongezea muda ajiongezee kwake huko chato gbadolite aifanye nchi yake atawale milele.

Mandingo Mlaza kifo cha Mende Kondoo atashinda kawe? Betina anawezana kumuondoa Sugu kweli?. "Kichaa Huru" huyo ndio hata tatu bora hayupo!!! Huyo Mnyeti hata kama ni chagua la JIWE wananchi washamkataa kabla hata ajachatueliwa kugombea!! Kwa Makonda 50% 50% inategemea hoja/mashambulizi na kulinda kura kutoka upinzani.
 
Tetesi

Members, wasibezwe hili kundi la CCM mpya na waongeaji watapita kwa kishindo kikuu kwa lengo maalum bungeni kubadili katiba na Kuongeza muda wa Rais kutawala

Kauli ya Rais mstaafu Mwinyi sio mara moja au kwa bahati mbaya anapenyeza kauli ya kubadili Katiba kuhusu ukomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Watu wafuatao ndio watakaoendesha bunge na kuwa waongeaji wakuu bungeni. Hakuna atakaye nyanyua mdomo wake kuwapinga watu wafuatao bungeni:

Paul Makonda
Cyprian Musiba
Alexander Mnyeti
Mchungaji Gwajima
Tulia Ackson

Waliotajwa wataingia bungeni kimkakati na siyo kwa bahati mbaya. Hoja zao ndio zitakuwa za mwisho kwa maamuzi ya Taifa.

Paul Makonda, Alexander Mnyeti, Mchungaji Gwajima na Cyprian Musiba msiwachukulie kirahisi na kuwadharau, Hao watu ni wajenga hoja wazuri tena za kulazimisha utake usitake lazima uwaunge mkono ili ubaki salama kwenye CCM mpya.

Hakuna cha mpasuko wala ufa CCM. Sauti ni moja tu yenye nguvu na kuheshimiwa. Hakuna mwenye uwezo wa kumpinga Mwenyekiti wa chama wala kunyanyua mdomo kuhoji maamuzi ya Mwenyekiti.

Mwenyekiti amepitishwa kwa asilimia 100%. Hii inampa nguvu ya kuaminiwa na yeyote atakaye ongea kuhusu kura za maoni kwa upande hasi hasa za ubunge basi atafute Maisha mengine nje ya bunge na CCM mpya.

CCM ni moja na yenye nguvu zaidi, Wapinzani tafuteni mbinu mpya, CCM imempa mamlaka ya asilimia 100% Mwenyekiti kwa kupiga kura za ndio Dodoma, Sauti yake ni sauti kuu. Hakuna mwanachama atakaye tenda nje ya Maamuzi ya Chama

Wapinzani msisubiri eti CCM kutakuwa na mpasuko ili mpate hoja za ubunge, Bunge linakwenda kuwa la kimkakati kupitisha hoja maalum ya ukomo wa Rais madarakani.

Mkuu uko sahihi sana, lengo la Magufuli ni kuongezewa muda wa kukaa madarakani, hilo angelifanya bila hata hao wabunge uliowataja kwenda huko bungeni. Kuna uzi nilisema jana humu, uchaguzi huu utakuwa ni wa hoja V/S bunduki, lengo ni kupata serikali inayotii amri ya mtu mmoja. Ila uzuri, uongozi sio lazima upatikane kwa njia ya kura tu. Njia ya kura ni njia ya amani, lakini sio njia pekee. Maadamu njia hii ya kura imepuuzwa na kunajisiwa, basi tutegemee njia mbadala wa kura kupata uongozi.
 
Ndio, tatizo wenye bongo wameungamishwa na kwamba wakipigwa kofi kushoto wanageuza kulia lije lingine baada hapo huingia kwenye mapambio ya sifa!
Imani mpya mseto!
 
Inaweza kuwa hivyo au isiwe. Inawezekana kina Makonda na Gwajima wanataka uwaziri, mpaka uwaziri Mkuu

Paul Makonda huwa anaamini siku moja atakuwa Rais wa nchi hii.
Believe me haitokaa itokee. Kwenye uwaziri hapo sawa
 
Ni point nzuri hizo
Ila kwani hata wakisema aongeze muda wa ukomo wa urais unadhani kuna mtu ataandama kulipinga hilo? Thubutu tulivyo waoga hivyo.. wale mlio karibu na kituo cha polisi Oysterbay mnaona yale yanayoendelea hivi karibuni milio ya risasi kila mara kama una pressure huwezi kuendelea kukaa maeneo yale ...walivyohoji kwanini wakaambiwa watu wapo matunzoni...daah sasa kama ile milio inasikika vile eti ni mafunzo si wangetoka nje ya mji kidogo ili kuepusha hofu kwa wananchi walio karibu na maeneo ya Oysterbay Morocco na Msasani
Binadamu ni kiumbe anayezoea na akishazoea anaamini, akishaamini anajihami na woga wote unamtoka. Ukitaka kuamini chukua binadamu, mfungie sehemu halafu kila siku ingia mpige kofi, kesho tena kofi fanya hivyo kwa muda halafu angalia respond yake kila muda unapokwenda.
 
Magufuli hataongeza hata dakika moja. Akithubutu lazima watanzania tukatae.
 
Jamani Mh. Rais kasema wazi, hawezi ongeza muda, muda wake ukiisha anaondoka zake, kwanini mnamsemea maneno ya uongo, lini Mh. Rais kasema anataka kuongeza muda? Huku ni kuchafuana, acheni hizo plz
 
Kuna kitu inaitwa "SHIKWAMBI"
Maana yake "Shinda kwa Mbinu "

Iwe Jua au Mvua, Iwe kelele au vicheko ccm itashinda kwa mbinu

Serikali za mitaa ilitumika mbinu inaitwa "KATA" maana yake katisha tamaa

Sasa uchaguzi mkuu ni mwendo wa "SHIKWAMBI"

Ahaaa Mshana huyajui Haya, Hujapata kuyasikia Haya

Na mwenye masikio na asikie, Hata hii mbinu ilipata tapakaa majimbo yote kuanzia kusini hata kaskazini kwa wenye roho ngumu nako ilipata kutumika

Ni nani mwenye kuhoji kazi nzuri zilizofanyika kwa miaka mitano, Ni wewe Mshana

Hujasikia habari kuu za SGR, Uchumi wa kati, Flyovers

Yote hayo ni sehemu ya Shikwambi
KAMA UNAFIKIRI CCM PEKE YAO NDIO WANAWEZA KUFANYA HIYO 'SHIKWAMBI' UMEPOTEA, THIS TIME CCM INAENDA KUAIBIKA KWA KISHINDO!
 
Back
Top Bottom