Wabunge wa CCM wanamshambulia Gwajima. Je, amefanya kipi kibaya?

Wabunge wa CCM wanamshambulia Gwajima. Je, amefanya kipi kibaya?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Wabunge wa CCM wanamshambulia Gwajima. Je, amefanya kipi kibaya?

Mwingine amediliki kusema Bungeni bila aibu kuwa vyombo vya dola vianze na wale waliopo ndani ya CCM kisha vimalizie wa nje ya CCM

Je, hichi ni chama sahihi kutawala Watanzania?

Yaani tunatawaliwa na Chama ambacho kinahimiza vyombo vya dola kuua raia badala ya kufuata misingi ya katiba na sheria za nchi.

Yaani wanaofanya makosa watekwe na kuuliwa badala ya kupandishwa Mahakamani?

Ni aibu kubwa taifa kuwa na Chama kama hiki.
 
Ccm tulioikulia haikuwa hivi. Ili jali sana wananchi hata ws nchi nyingine. Ilikemea udikteta hata wa nchi nyingine. Ndiyo maana ilijitolea hata kutuma majeshi ya ukombozi kwa nchi hizo.

Tangu Ccm ibaki kuongozwa na wapiga dili. Imebadili muelekeo na yenyewe kuwa ya ki dictator kuliko madictator wenyewe. Na sasa hawataki wananchi wafurukute bali waufyate.
 
Hii ni ajabu sana Yani hakuna hata mmoja aliyepangua Hoja ya Gwajboy badala yake wanashambulia Kwa mfano Kuna mbunge alisema Gwajiboy alipaswa kuyasema hayo ndani ya chama na Si Nje(public)

Tunaongozwa na wapiga dili si vingine
 
Mkuu, kwa mujibu wa Wakenya, Gwajima kagusa ^mrima!^

Hutakiwi kucheza kabisa na ^watu wa mrima!^
 
Tangu CCM ilipokabidhiwa kwenye uongozi wa kishetani, kimekuwa chama cha shetani, chama cha kuwaangamiza watanzania.
 
Ulishawahi kuona mtu anakujibu bila kukusikiliza? Nina mashaka hao hawajasikiliza hotuba ya Gwajima. Hata ukimuuliza anamjibu Gwajima juu ya nini haelewi
 
WAMESAHAU KUWA MKUBWA NI JALALA...LAKINI WENGINE WANATAFUTA VYEO..GWAJIMA KAJA KULUDISHA IMANI YA WANANCHI KWA VYOMBO VYAO VYA ULINZI NA USALAMA KUTOKANA NA MFULULIZO WA MATUKIO YANAYOENDELEA NA KUTOA MIFANO HAI WAO WANAMSHAMBULIA KWA MANENO BADALA YA KUPINDUA KWA HOJA NA MIFANO HAO NDO WANAOTUHARIBIA NCHI YETU KWA KUTETEA MATUMBO YAO BADALA YA MASLAHI YA WANANCHI.
 
Ccm tulioikulia haikuwa hivi. Ili jali sana wananchi hata ws nchi nyingine. Ilikemea udikteta hata wa nchi nyingine. Ndiyo maana ilijitolea hata kutuma majeshi ya ukombozi kwa nchi hizo.

Tangu Ccm ibaki kuongozwa na wapiga dili. Imebadili muelekeo na yenyewe kuwa ya ki dictator kuliko madictator wenyewe. Na sasa hawataki wananchi wafurukute bali waufyate.
Nimetafakari sana ya Gwajima. Ujumbe wake inawezekana kuna mahali panahitaji msaada wa wananchi wao waanze kazi.
 
Back
Top Bottom