Masanilo,
Kama una guts toa jina lako kamili na ndio tujadiliane na haitachukua muda kujua nani fisadi zaidi.
Umetumia muda wako mwingi kumchafua Mwakalinga hapa JF, sishangazwi na comments zako. Unaweza kuniita fisadi au fisadi mtoto utakavyo, ila ambacho hutaweza kufanya ni kuonyesha fact yoyote ambao inaonyesha Mwakalinga ni fisadi au kamwibia nani? Zaidi ya nusu za posts zako 5000, ni maendelezo ya chuki na wivu uliozidi kiasi dhidi ya Mwakalinga.
Endelea na kuchafua wana JF wengine, lakini pia tuambia wewe umefanya nini hata kidogo cha kuisaidia Tanzania mpaka uwe arrogant kiasi hicho?
Huwezi kuhama Kyela kwasababu hutoki Kyela. Any way siwezi kuvunja sheria za JF, ila hao wanafunzi wako wana kazi kubwa kweli. Inaelekea una wivu wa kijinga. Sitapoteza muda wangu kubishana na mtu ambaye ameonyesha chuki kubwa kiasi hicho bila kutoa sababu hata moja.
Vinginevyo nakuweka kundi la Watanzania walio wengi ambao hawasaidii wenzao, hawafanyi lolote la maana zaidi ya kujaza matumbo yao na wanaongoza kueneza majungu ya kuchafua wale wanaofanya tofauti na wao.
Endelea haitaninyima hata tone la usingizi maana nakufahamu vizuri na huna hata kura moja Kyela.